Habari za Punde

Kozi ya Makocha wa magolikipa yafungwa

Makocha wa Magolikipa walioshiriki katika kozi maalum wakiwa katika picha ya pamoja

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Kozi ya awali ya Makocha wa makipa visiwani Zanzibar imefungwa asubuhi ya leo na mkurugenzi wa ufundi wa ZFA Taifa Abdulghani Msoma, hafla ambayo imefanyika kwenye ukumbi wa uwanja wa Amaan.

Kozi hiyo imechukua siku 7 ambapo ilianza Jumatano ya July 5 na kuhutimishwa leo hii chini ya mkufunzi wa makipa Saleh Ahmed Seif “Machupa” na ilijumuisha makocha 29.

Akizungumza na mtandao huu, mara baada ya kumalizika kwa kozi hiyo, mkurugenzi wa ufundi ZFA Taifa Abdul ghani Msoma ameeleza zaidi umuhimu wa vilabu kuwa na makocha wa makipa ili watumike kwenye vilabu vyao.

Mtandao huu hatukiishia hapo, ukazungumza na makocha wa makipa waliohitimu kozi hiyo ambapo kocha Salum Ali Chulas wa KMKM kwa niaba ya wenzake amewaomba ZFA kuweka sheria maalum ili timu za ligi kuu ziwe na makocha wa Makipa waliosoma kozi maalumu za makocha wa makipa.

Makocha 29 wa Magolikipa waliofanikiwa kupata kozi hiyo ni pamoja na Shija Elius Simon (Uhamiaji), Hassan Abdul-rahman Said (Zimamoto), Twahir Ahmada Mzee (Al-Kamal), Yousuph Saleh Abdul-hamid (Chuoni), Nasri Ally Maulid (Maungani), Kombo Khamis Kheri (Jang’ombe Boys), Khamis Uzidi Omary (Zimamoto), Shaibu Ismail Juma (Negro FC), Ayoub Frank (Mafunzo) na Farijala Juma Ramadhan (JKU).

Wengine ni Khamis Suleiman Shaaban (Idumu FC), Abdillah Juma Silima (Black Sailors), Said Abdallah Ali (Kitase), Maulid Makame Tabu (Urafiki), Abdulla Ali Hemed (Kitase), Omar Said Hamad (Kwalinato), Ali Maulid Haji (KVZ), Khamis Haji Juma (KVZ), Juma Ali Aboud (Kundemba), Jaffar Iddi Masoud (Kipanga), Mohammed Khamis Ally (Kipanga), Abdulnasir Ahmada Mzee (Kilimani City), Othman Mohd Mohd (Bweleo), Abdul-hamid Khamis Faki (Miembeni), Mnyupe Said Mfaume (KMKM), Salum Ali Salum (Black Sailors), Abass Nassor Ali (Taifa ya Jang’ombe) na Farouk Ramadhan Mzee (Al-Mudhaib).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.