Habari za Punde

Ligi Kuu ya Zanzibar Nane Bora Kati hya Jamuhuri na Jangombe Boys Mchezo Uliofanyika Uwanja wa Amaan Timu ya Jangombe Boys Imeshinda Bao 1--0. T

Beki wa Timu ya Jangombe Boys akirusha daruga juu mbele ya mshambuliaji wa Timu ya Jamuhuri katika eneo la kuminane na kudai kunyimwa peneti kutokana na mchezo wa beki huyo iliofanya mchezaji huyo kukimbizwa huspitali kupata huduma ya kwanza baada ya kupata majaraha na kuwekewa waya katika meno yake ya mbele kutokana na fauu hiyo. Kwa mujibu wa Kocha wa Timu huyu amesema mchezaji wake amewekewa waya kuzuiya meno ya mbele ya mchezaji wake na kunyiwa peneti kutoka na mchezo huo mbaya aliochezewa mchezaji wake, Katika mchezo huom Timu ya Jangombe Boys imetoka na ushindi wa bao 1--0.
Wachezaji wa Timu ya Jamuhuri kulia na Jangombe Boys wakiwania mpira wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar Nane Bora mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar. 

Wachezaji wa Timu ya Jangombe Boys wakishangilia bao lao la kwanza na laushindi dhidi ya Timu ya Jamuhuri wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar Nane Bora uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar.
Wachezaji wa Timu ya Jangombe Boys wakishangilia bao lao.
Wachezaji wa Timu ya Jamuhuri wakimzonga muamuzi wa mchezo huo kwa kudai bao walilofunga sio halali halikuingia wavuni kutokana na kipa wa timu hiyo kuokoa mpira huo. ukiwa unaelekea wavuni. Wachezaji wa Timu ya Jamuhuri wakimlalamikia muamuzi wa mchezo huo baada ya mchezaji wao kuchezea rafu akiwa katika eneo la goli la Timu ya Jangombe Boys na kudai kupewa peneti.


Kocha Mkuu wa Timu ya Jamuhuri akiwa na simazi kutokana na Timu yake kupoteza mchezo huo dhidi ya Timu ya Jangombe Boys uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar.Kushoto Kocha Mkuu wa Timu ya Jangombe Boys akimfariji Kocha Mkuu wa Timu ya Jamuhri kushoto baada ya kumalizika kwa mchezo huo wa Ligi Kuu ya Zanzibar Nane Bora uliofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar. Timu ya Jangombe Boys imeshinda bnao 1-0.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.