Habari za Punde

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Ayoub Azindua Michuano ya Kipwida Cup

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Mashindano ya Kipwida CUP yameanza rasmi jioni ya leo katika uwanja wa Lion Kids kwa mchezo kati ya Kisakasaka United na Big Nation uliomalizika kwa Kisakasaka kufungwa mabao 2-1, ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud.

Kisakasaka ndio waliotangulia kupata bao katika dakika ya 12 kupitia kwa Abdillah Ali na kusawazishiwa dakika ya 77 kupitia kwa Ramadhan Yussuf ambae alifunga ena dakika ya 82.

Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea tena kesho kwa mchezo mmoja kati ya Basra Boys dhidi ya Mpira Pesa katika Uwanja wa Lion Kids saa 10 za jioni.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.