Habari za Punde

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Azindua Bodi Mpya ya Ushuru ya Wizara - Taasisi ya Uhasibu Tanzania.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa  Bodi mpya ya Ushauri ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA). Uzinduzi huo umefanyika hivi karibuni katika kampasi ya TIA Singida mjini. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi mpya ya Ushauri TIA Said Chiguma na Afisa Mtendaji Mkuu wa TIA Joseph Kihanda na kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe. Elias Tarimo na Mjumbe wa Bodi Dkt. Leonada.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Joseph Kihanda, akitoa nasaha zake kwenye hafla ya uzinduzi wa Bodi mpya ya Ushauri ya Taasisi hiyo. Uzinduzi huo umefanyika hivi karibuni katika kampasi ya TIA tawi la Singida mjini.  
Mwenyekiti wa Bodi mpya ya Ushauri ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Said Chiguma akizungumza kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa Bodi mpya ya Ushauri ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA). Uzinduzi huo umefanyika hivi karibuni katika kampasi ya TIA tawi la Singida mjini. 
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa  Bodi mpya ya Ushauri ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA). Uzinduzi huo umefanyika hivi karibuni katika kampasi ya TIA Singida mjini. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi mpya ya Ushauri TIA Said Chiguma na Afisa Mtendaji Mkuu wa TIA Joseph Kihanda na kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe. Elias Tarimo na Mjumbe wa Bodi Dkt. Leonada.

NA: MWANDISHI WETU
SINGIDA
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango  Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amezindua Bodi mpya ya Ushauri ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kwa lengo la kuimarisha ufanisi wa Taasisi  na uangalizi wa karibu.

Akizungumza hivi karibuni wakati wa uzinduzi huo uliofanyika  Taasisi ya Uhasibu Tanzania kampasi ya Singida  Dkt. Kijaji amesema Bodi hiyo itamsaidia Waziri wa Fedha na Mipango kupata ushauri wa kitaalam  na hatimaye kutoa maamuzi  yenye tija kwa Taasisi na Taifa kwa ujumla.

"Bodi hii ya Ushauri inategemewa kutoa mchango  wa mawazo na  kitaalam yanayohusu uendeshaji  na uboreshaji wa  Taasisi yetu ya TIA ili kuendana na mabadiliko yanayoendelea duniani katika nyanja mbalimbali za kiuchumi, kiteknolojia, kisiasa na kijamii", amesema Dkt. Kijaji.

Dkt. Kijaji ameongeza kuwa Bodi hiyo ina wajibu wa kujua ubora wa wanafunzi wanaohitimu katika chuo hicho ikiwa ni pamoja na ubora wa vyeti vyao kuendana na uwezo wao wa kufanya kazi katika fani walizosomea na kukabiliana na changamoto kwenye maeneo ya kazi.

Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania Said Chiguma amesema Taasisi hiyo inakabiliwa na changamoto ya uchache wa miundombinu kama vile kumbi za mihadhala, madarasa, maktaba na maabara za kompyuta ambavyo ni nyenzo muhimu katika utoaji wa elimu iliyo bora.

Chiguma amesema ili kupunguza changamoto hizo, Taasisi inajitahidi kutenga fedha inazozikusanya ili kukarabati na kujenga majengo mbalimbali kwa ajili ya kuboresha elimu na kuongeza uwezo wa kudahili wanafunzi wengi zaidi.

Taasisi ya Uhasibu Tanzania ni chuo cha Serikali ambacho kinatoa mafunzo katika fani za Uhasibu, Ununuzi na Ugavi, Usimamizi wa Biashara, Uongozi wa Rasilimali Watu, Masoko na Uhusiano wa Umma pamoja na Uhasibu wa Fedha za Umma kuanzia ngazi ya Astashahada (Certificate), Stashada (Diploma)  na Shahada (Degree).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.