Habari za Punde

Utata wa suala la kodi ya Majengo




Moja ya ahadi tuliopewa hivi karibuni ni kuwa TRA mpya yenye taratibu na mipango inayoeleweka. Kuna safu mpya kabisa ya uongozi na mifumo mpya. Sadakta. Kama miaka miwili iliyopita lilifanyika zoezi la kufanya tathmini ya maeneo Kinondoni. 

Nimelifuatilia kwa karibu na sijaona tamati yake. Kila nikiuliza naambiwa nitatumiwa barua. 

Siku zimeenda nimelipa kodi yangu ya ardhi ya jengo tata. Nimekwenda huko TRA kufuatlia naambiwa jina langu halipo katika system nikaambiwa nenda katika kanda kilipo kibanda changu. Huko hadithi hiyo hiyo. Nikaambiwa npigie picha kibanda changu nipeleke. Itasaidia kufanya tathmini.

Suali sehemu zote naulizwa unataka kulipa ngapi?

Kama niseme tu ilikua na maana gani kufanya zoezi la tathmini ya majengo? Je kuna vigezo vya kuzingatia kwa kuweka viwango vya malipo yaani formula?. 

Kwanini isitumike tukaanza hapo? Nkisema kubwa ntaumia nkisema ndogo ntaumia.

Nkaambiwa pia nipate barua serikali ya Mtaa. Serikali ya Mtaa wakataka kujua namba yangu ya nyumba ambayo mpaka sasa wanajua hawajanipa licha ya kuwa nishailipia na mpaka lei risiti hawajatoa.

Hitimisho langu wakati natafakari hatma ya kodi ya majengo ni wazi kuwa Tanzania bado tupo na utamaduni ule ule wa kukurupuka,kusumbua watu wakati miundo mbinu na mipango hayako sawa....sasa wanaolipa wanalipa viwango halali au ndo kukamuana?

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.