Habari za Punde

ZRB Yatowa Elimu ya Mashine za Kielotronic Kwa Waandishi wa Habari Kisiwani Pemba.

Na Salmin J. Salmin Pemba.
Bodi ya mapato Zanzibar ZRB imewataka wafanyabiashara kuwa tayari kuzipokea na kuzitumia mashine za utoaji risiti za kielectronic (EFD) zinazotarajiwa kufungwa hivi karibuni ili kuondokana na usumbufu wa ukusanyaji kodi unaojitokeza.
Hii ni kutokana na kuwepo kwa mfumo wa utoaji wa risiti kwa mkono ambao unaonekana kuwa na matatizo mengi na kupelekea kuikosesha serikali mapato yake.
Akito mafunzo kwa wandishi wa habari huko katika ukumbi wa kiwanja cha Gombani chakechake juu ya matumizi ya mashine hizo mkuu wa idara ya sera utafiti na mipango ZRB Nd, Khamis Saadat, amesema utoji wa risiti kwa kutumia mashine za kielectronic ni mfumo wa kisasa ambao unatumika katika kutunza kumbukumbu na kuondoa udanganyifu katika ulipaji kodi kwa wafanya biashara.
Amefahamisha kuwa mfumo huu utamuezesha mteja kupatiwa risiti halali yenye kuonesha uhalali wa bidhaa aliyonunua pamoja na bei aliyonunulia.
Kwa upande wake mkuu wa idara ya teknologia ya mawasiliono (ICT) Nd, Mussa Amour Ali amesema wafanya biashara walikuwa na uwezo wa kuichezea mifumo ya zamani ya utoaji risiti na kupelekea kukosekana kwa mapato lakini kwa mfumo huu wa kisasa hawatoweza kufanya hivyo kwani mashine hizo zitakuwa zinaendeshwa na ZRB wenyewe.
Amefahamisha kuwa endapo mfanya biashara hatopeleka taarifa za mauzo kwa ZRB basi badi hiyo itapata ripoti zote kupitia mashine yake hiyo.
Mkuu huyo amesema mashine hizo hawatafungiwa wafanya biashara tu bali maeneo yote hadi kwenye taasisi za serikali ili kuzuia mwanya wa ukwepaji kodi

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.