Habari za Punde

Mkutano wa Wadau wa Kuelimisha Sekta ya Uchukuzi Juu ya Mpango wa Taifa wa Utafutaji na Uokoaji "Search And Rescue Plan" t

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Bahari Zanzibar (ZMA) Abdallah Kombo akizungumza na kufungua mkutano wa siku moja kwa Wadau wa sekta ya usafiri wa baharini na nchi kavu na vyombo vya ulinzi na usalama Kuelimisha Wadau wa Sekta ya Uchukuzi Juu ya Mpango wa Taifa wa Utafutaji na Uokoaji "Search And Rescue Plan" mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa zamani wa baraza la wawakilishi kikwajuni Zanzibar. 


Kaimu Mkurugenzi Usalama na Mazingira Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Tanzania Bi Stella Joshua Katondo akizungumza wakati wa mkutano huo wa Wadau wa Sekta mbalimbali kuhusiana na Uokoaji na Utafutaji uliofanyika katika ukumbi wa zamani wa baraza wawakilishi kikwajuni Zanzibar na kuwashirikisha wadauy wa usafiri wa baharini na vyombo vya ulinzi na usalama Zanzibar. 
Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia kwa makini. 
Watoa Mada wakifuatilia wakati wa ufunguzi wa mkutano huo katika ukumbi wa baraza la wawakilishi la zamani kikwajuni Zanzibar.


Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Zanzibar wakifuatilia mkutano huo kwa makini.  
Mkurugenzi Wizara ya Mawasiliano Zanzibar Rajab Uweje akizungumza na kutowa taarifa wakati wa mkutano huo. 

Mtoa Mada kutoka Taasisi ya TCAA Afisa Mkuu wa Utafutaji na Uokozi Katika Safari za Ndege Norbert Bwire akitoa mada wakati wa mkutano hau na wadau wa mbalimbali walioshiki katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa zamani wa baraza la wawakilishi kikwajuni Zanzibar.
Afisa kutoka Sumatra Mkuu wa Kitengo cha Utafutaji na Uokozi Alex Katama akitowa ufafanuzi wakati wa mkutano huo baada ya kuwasilishwa mada na muhusika.  




No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.