Habari za Punde

Kambi ya Wanamichezo Majeshi wa Tanzania Yaendelea Vyema Kisiwani Zanzibar.

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Mashindano ya Majeshi ya Michezo ya Afrika Mashariki na Kati mwaka huu yatafanyika Bujumbura Mjini Burundi kuanzia  Agost 20, 2017 ambapo timu za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) litashiriki kwa michezo mitano ikiwemo mpira wa Miguu, mpira wa Kikapu, mpira wa Wavu, mpira wa Pete na Riadha.

Timu hizo za JWTZ zimeweka kambi Visiwani Zanzibar ambapo kambi hiyo inaendelea vizuri mpaka sasa huku wakipania kutwaa ubingwa.

Akizungumza na Mtandao huu Kanal Mwandike ambae ni Mkurugenzi wa Michezo wa JWTZ amesema kambi inaendelea vizuri Zanzibar na  wamepania kufanya kweli mwaka huu.

“Kambi inaendelea vizuri hapa Zanzibar na hakuna tatizo lolote mpaka sasa, tumeshacheza michezo mbali mabli ya kirafiki na timu zinaonesha kiwango cha hali ya juu kabisa, mwaka huu tumepania kufanya vyema kuliko mwaka jana, mbi ana mwaka jana tulishinda nafasi ya pili lakini mwaka huu tutakuwa wa kwanza”. Alisema Kanal Mwandike.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.