Habari za Punde

Kocha Mkuu wa Timu ya Jamuhuri Apata Kibarua Ligi Kuu ya Vodacom Bara.



Na: Abubakar Khatib “Kisandu”, Zanzibar.

Klabu ya Ruvu Shooting imemteua Abdul mutik Haji (Kiduu) kuwa kocha mpya wa timu yao na kumpa mkataba wa mwaka mmoja, ambapo anaweza akaongezewa miaka mengine akifanya vizuri.

Kiduu mwenye leseni A ya CAF alikuwa Kocha Mkuu wa timu ya Jamhuri ambao ndio vinara wa ligi kuu soka ya Zanzibar na ameondoka hapo Jamhuri baada ya kuagalia maslahi bora ziaidi Ruvu.

Akithibitisha taarifa hizo Kocha Kiduu amesema ni kweli amejiunga na Ruvu na sasa akili yake yote ni kujipanga kuhakikisha timu yake mpya inaleta upinzani mkubwa zaidi katika ligi kuu soka ya Tanzania bara.

“Ni kweli nipo Ruvu na nimefunga mkataba wa mwaka mmoja, kwasasa najipanga kuhakikisha Ruvu inafanya vizuri zaidi ya msimu uliopita katika ligi kuu bara”. Alisema Kiduu.

Kiduu amechukua nafasi ya Malale Hamsini keya aliyekwenda Ndanda FC ya Mtwara ambapo pia alikuwa ni Mzanzibar kufundisha timu hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.