Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Akitowa Mkono Pole Kwa Kifo cha Kiongozi wa Chama cha TADEA Marehemu John Chipaka.


Na. Othman Khamis OMPR.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetoa mkono wa pole kwa Chama cha Siasa cha ADA-TADEA Taifa  kufuatia kifo cha Mwenyekiti wa Chama hicho Mzee John Lisa Chipaka.


Salamu hizo zimewasilishwa na Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Wazizi asiye na Wziaara Maalum wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mh. Juma Ali Khatibu wakati wa mazishi ya Mwanasiasa huyo Mkongwe Tanzania yaliyofanyika leo mchana katika Makaburi ya Kindondoni Jijini Dar es salaam.

Mh. Juma Ali Khatibu amemuwakilisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwenye msiba huo uliogusa nyoyo za Wanachama wa Chama cha ADATADEA pamoja na Watanzania walio wengi Nchini.

Mzee John Lisa Chipaka  ni miongoni mwa Wanasiasa wakongwe Nchini Tanzania waliotoa mchango mkubwa katika harakati za Tanzania kuingia katika mfumo wa vyama vingi vya Siasa mnamo mwaka 1992. Katika harakati za kisiasa Mzee Chipaka alikuwa Mjumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania  nafasi aliyoitumikia kwa juhudi na umahiri
mkubwa hadi kufariki kwake.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Wananchi wa Zanzibar  wameupokea kwa huzuni msiba huo na kuwataka Wanachama wa ADA -TADEA pamoja na familia ya Marehemu kuwa na moyo wa subira katika kipindi hichi cha msiba. Mwenyezi Muungu ailaze royo ya Marehemu Mzee John Lisa  Chipaka mahali pema peponi. Amin.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.