Habari za Punde

Mchezaji Bora wa Zanzibar Asainiwa Ligi Kuu wa Vodacom Bara..

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Mchezaji bora wa Mwezi Novemba wa ligi kuu soka ya Zanzibar msimu wa mwaka 2016-2017 Majid Khamis “Dudu” amesaini kandarasi ya mwaka mmoja kuichezea klabu ya Ndanda FC ya Mtwara akitokea Black Sailors.

Dudu ambae anacheza nafasi ya kiungo mshambuliaji amefurahishwa mno kusajiliwa na timu inayoshiriki ligi kuu soka Tanzania bara ambapo akitegemea kuonesha kiwango cha hali ya juu kwenye timu hiyo.

“Unajua Zanzibar kuna vipaji vingi sana, naamini namimi ntaonesha kipaji changu katika ligi kuu ya bara, malengo yangu ni kufika mbali zaidi ya hapa nilipofika sasa, nawashukuru Black Sailors kwa kunilea vizuri hasa hasa kocha wangu Juma Awadh pamoja na benchi zima la ufundi na wachezaji wenzangu wote wa Sailors”. Alisema Dudu.

Idadi ya Wachezaji kutoka Zanzibar kwenda kucheza ligi kuu soka Tanzania bara inazidi kuongezeka baada ya wachezaji kadhaa wakiwemo Abdallah Haji Shaibu “Ninja” aliyesajiliwa Yanga akitokea Taifa ya Jang’ombe, Ibrahim Mohammed “Sangula” aliyesajiliwa Ndanda akitokea Jang’ombe Boys, Ali Hamad “Kidimu” kaenda Stand United kuhama Gulioni FC pamoja na Dudu huyo alotoka Black Sailors kujiunga na Ndanda FC.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.