Habari za Punde

Michuano ya Nusu Fainali Kombe la Majimbo Cup Kuanza Kesho Jumamosi.

Na: Abubakar Khatib “Kisandu”, Zanzibar.

Mashindano ya Majimbo ya Unguja hatua ya Nusu fainali itapigwa kesho Jumamosi Agost 5, 2017 kati ya Jimbo la Mji Mkoongwe dhidi ya Afisi kuu ya CCM Kisiwandui saa 10:00 za jioni katika uwanja wa Amaan.

Kwa mujibu wa mratibu wa Mashindano hayo Uledi Said amesema mechi hiyo itakuwa bila ya kiingilio.

“Matayarisho yamekamilika mechi nusu ya kwanza itachezwa Jumamosi nay a pili Jumapili na hakuna kiingilio”. Alisema Uledi.

Nusu fainali ya pili itapigwa Jumapili Agost 6, 2017 kati ya Jimbo la Kwahani dhidi ya Kikwajuni saa 10:00 za jioni katika uwanja wa Amaan.
Bingwa wa Mashindano hayo atazawadiwa gari aina ya Carry.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.