Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akionesha Ramani ya Ujenzi wa Mji wa kisasa utakaojengwa sambamba na ufukiaji wa Bahari ya Eneo la pwani ya Gulioni katika kikao cha siku moja kilichojumuisha Uongozi wa Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Nyumba na Uongozi wa Shirika la Nyumba katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo,[Picha na Ikulu.] 01 /08/2017.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akionesha Ramani ya Ujenzi wa Mji wa kisasa utakaojengwa sambamba na ufukiaji wa Bahari ya Eneo la pwani ya Gulioni katika kikao cha siku moja kilichojumuisha Uongozi wa Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Nyumba na Uongozi wa Shirika la Nyumba katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo,[Picha na Ikulu.] 01 /08/2017.
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Nyumba wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) wakati alipofanya kikao cha siku moja pamoja na Uongozi wa Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo,[Picha na Ikulu.] 01 /08/2017.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Nyumba na Uongozi wa Shirika la Nyumba katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo,[Picha na Ikulu.] 01 /08/2017.
STATE
HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF
THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar
01.08.2017
RAIS wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, amesema kuwa kuwepo kwa mabadiliko makubwa ya
kimaendeleo baada ya kuundwa kwa Mamlaka ya Viwanja vya ndege vya Zanzibar kumeweza
kuongeza mapato na kuahidi kuimarika zaidi hali hiyo ndani ya kipindi chake cha
uongozi.
Dk. Shein aliyasema hayo leo,
alipokutana na uongozi wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji, Bodi
ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege pamoja na Uongozi wa Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege katika vikao vinavyoendelea Ikulu mjini Zanzibar.
Dk. Shein alitumia fursa
hiyo kuipongeza Mamlaka hiyo kwa kufanya mabadiliko makubwa katika viwanja vya
ndege vya Zanzibar hatua ambayo imeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa ongezeko la
mapato katika viwanja hivyo.
Katika maelezo yake Dk.
Shein alisema kuwa licha ya baadhi ya changamoto zilizopo lakini Mamlaka imeweza
kupata mafanikio makubwa na hivi leo viwanja vya ndege Unguja na Pemba viweza
kuimarika na kuleta tija kwa kuongeza mapato.
Akizungumza suala zima la
fidia kwa wananchi waliojenga pembezoni mwa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa
Abeid Amani Karume Zanzibar Dk. Shein alisema kuwa ni vyema likatafutiwa
ufumbuzi kwa kuwatafuta wahusika na kuwasikiliza madai yao ili hatua za malipo
ziendele kuchukuliwa.
Akizungumza na uongozi wa
Wizara hiyo kupitia Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Nyumba pamoja na Uongozi
wa Shirika hilo, Dk. Shein alisisitiza haja ya Shirika hilo kuzitambua na
kuziorodhesha ili kujua idadi ya nyumba zao zote za Unguja na Pemba pamoja na
zile za Wakala hatua ambayo pia, itasaidia kuepusha udanganyifu.
Dk. Shein alitumia fursa
hiyo kutoa pongezi kwa Bodi ya Shirika hilo pamoja na uongozi wa Shirika hilo
kwa mafanikio makubwa yaliopatikana kwa
kipindi kifupi.
Alieleza haja ya kuwepo
utaratibu wa kuwatambua wakaazi wananoishi katika nyumba zote za Mji Mkongwe wa
Zanzibar ili iwe rahisi katika kutekeleza mipango ya Serikali huku akieleza
azma ya Serikali ya kujenga miji ya kisasa sambamba na kutekeleza mradi wa
kufukia bahari katika eneo la pwani ya Gulioni kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za
kisasa zikiwemo hoteli.
Wakati
huo huo,
Dk. Shein alikutana na uongozi wa Wizara hiyo walioongozana na Bodi ya
Wakurugenzi ya Mamlaka ya Uhifadhi na Uendelezaji Mji Mkongwe na Uongozi wa
Mamlaka ya Uhifadhi na Uendelezaji Mji Mkongwe na kueleza umuhimu wa kuweka utaratibu
maalum juu ya kupunguza foleni ya gari katika barabara inayopita katika Bandari ya Malindi.
Aidha, alieleza haja ya
kuzingatia na kufuata kanuni na misingi ya Sheria iliyounda Bodi hiyo ili
Mamlaka hiyo na Bodi yake iweze kufanya kazi kwa ufanisi pamoja na kufuata
Sheria nyengine zote muhimu huku akieleza umuhimu wa uhifadhi wa mji huo.
Nae Makamo wa Pili wa Rais
wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd alieleza kwamaba tabia ya kukodishwa nyumba kwa
kutumia vilemba ambapo hatua hiyo ndio chanzo kikubwa cha upotevu wa nyumba za
Serikali huku akisikitishwa na baadhi ya wananchi waliopewa nyumba na Serikali
na wao kuzikodisha ama kuziuza bila ya kufuata taratibu na sheria zilizopo.
Waziri wa Wizara ya
Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Balozi Ali Karume kwa upande wake alieleza
hatua zzinazoendelea kuchukuliwa katika Wizara yake katika kutoa ushirikiano
uliopo kwa viongozi, wafanyakazi, Bodi pamoja na wajumbe wake.
Katibu Mkuu Kiongozi na
Katibu wa Baraza la Mapinduzi Abdulhamid Yahya Mzee kwa uonde wake alisisitiza
haja ya kuimarisha usalama katika viwanja vya ndege vya Zanzibar kwani
Mashirika ya ndege na hata wageni hilo wamekuwa wakilipa kipaumbele.
Mwenyekiti wa Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege Zanzibar Abdulhani Msoma aalieleza kuwa mapato yanayokusanywa
katika viwanja vya ndege yameongezeka kutoka TZS Bilioni 12.9 mwaka 2011/2012
hadi kufikia TZS Bilioni 39.3 mwaka 2016/2017.
Alieleza kuwa idadi ya
mashirika ya ndege imeongezeka kutoka mashirika 63 mwaka 2011 hadi mashirika 78
mwaka 2016 ambapo kati ya mashirika hayo, mashirika ya kimataifa yameongezeka
kutoka 39 mwaka 2011 hadi 48 mwaka 2016 na mashirika 24 ya ndani yameongezeka
hadi kufikia 30 mwaka 2016.
Aliongeza kuwa idadi ya
abiria imeongezeka kutoka 753,971 mwaka 2011 hadi abiria 1,032,043 mwaka 2016
sawa na asilimia 137 kati ya abiria hao abiria wa kimataifa wameongezka hadi
kufikia 529,696 mwaka 2016 kutoka abiria 283,755 mwaka 2011.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika
la Nyumba la Zanzibar Mohamed Hafidh Rajab alisema kuwa licha ya uchanga wa Shirika
hilo lakini ukusanyaji wa mapato yataongezeka kutoka TZS bilioni 1.6 mwaka
2017/2018 hadi kufikia TZS bilioni 48 katika mwaka 2021/2022 huku akieleza azma
ya ujenzi wa nyumba za makaazi zikiwemo za wananchi wenye kipato cha chini.
Nao uongozi wa Mamlaka ya
Uhifadhi na Uendelezaji Mji Mkongwe na Bodi yake ulieleza kuwa baadhi ya
Mashirika ya Umoja wa Mataifa pamoja na washirika wa maendeleo wameonesha azma
ya kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kuuimarisha Mji Mkongwe wake ikiwa
ni pamoja na kuzifanyia ukarabati mkubwa baadhi ya nyumba huku ukieleza hatua
zilizofikiwa katika utekelezaji wa miradi yake.
Katika vikao vya leo, Dk.
Shein alikutana na Uongizi wa Wizara hiyo pamoja na Bodi ya Wakurugenzi ya
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, uongozi wa Mamlaka pamoja na Bodi ya Shirika la
Nyumba na Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Uhifadhi na Uendelezaji Mji Mkongwe
na uongozi wake.
Rajab
Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax:
024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment