Habari za Punde

Raza Lee Awapa Jezi Waamuzi wa Wilaya ya Magharibi B Unguja.

Na: Abubakar Khatib “Kisandu”, Zanzibar.

Mfanyabiashara Mohd Ibrahim “Raza Lee” ambae ni mdau mkubwa wa michezo amewasaidia jezi 12 waamuzi wa ZFA Wilaya ya Magharibi B  .

Jezi hizo ambazo amekabidhiwa Ramadhan Keis ambae ni Katibu wa Waamuzi wa ZFA Wilaya ya Magharib B ambapo zoezi hilo limefanyika mchana wa jana katika Duka la Raza Lee ambapo linauza Vifaa vya Michezo liliopo Darajani Mjini Unguja.

Akizungumza na Mtandao huu Raza Lee baada ya kuwapatia Jezi hizo, amesema aliwapa ahadi Waamuzi hao na ndio mana jana akaitekeleza.

“Niliwahi kuwaahidi Waamuzi hawa kuwa ntawapatia sare, nashkuru Mungu leo (Jana) nimewakabidhi”. Alisema Raza Lee.

Kwa upande wake Ramadhan Keis ambae ni Katibu wa Waamuzi wa ZFA Wilaya ya Magharib B kwa niaba ya Waamuzi wenzake amefurahishwa mno kwa kupatiwa jezi hizo huku akiwaomba wadau wengine wajitokeze kuwasaidia.

“Tumefurahi kupatiwa vifaa hivi, tunaomba wadau wengine wajitokeze kutusaidia kwani waamuzi tupo katika wakati mgumu wakati mwengine ata sare hatuna, viatu na vifaa vyengine”. Alisema Keis.

Chama cha Soka Wilaya ya Magharibi B kina jumla ya Waamuzi 12 ambao wanasimamia Mashindano yao yakiwemo ligi Daraja la Pili na la Tatu Wilaya ya Magharibi B.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.