Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (wapili
kushoto) akiwasili na kupokelewa na Mtendaji Mkuu Taasisi ya Sanaa na Utamaduni
Bagamoyo (TaSUBa) Dkt. Herbert Makoye (kulia) wakati wa uzinduzi wa Tamasha la
36 la Sanaa na Utamaduni la kimataifa Bagamoyo Jana katika Taasisi hiyo.
Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya ushauri ya TaSUBa Bw. George Yambesi.
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (wapili
kulia) akimsikiliza mjasiriamali wa kazi za sanaa kutoka Dar es Salaam Bibi.
Magreth Kabonge (kushoto) alipotembelea banda lake kabla ya kufungua Tamasha la
36 la Sanaa na Utamaduni la kimataifa Bagamoyo jana katika Taasisi ya TaSUBa.
Kulia ni Mtendaji Mkuu Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Dkt.
Herbert Makoye
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.
Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akiangalia moja ya kazi za sanaa
iliyotengenezwa na mbunifu kutoka Arusha Bi. Joyce Lema (kushoto) alipotembelea
banda lake kabla ya kufungua Tamasha la 36 la Sanaa na Utamaduni la kimataifa
Bagamoyo jana katika Taasisi ya TaSUBa.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.
Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akionyesha picha yenye mfano wa sura yake
iliyochorwa na kalamu ya risasi na mwanafunzi kutoka Taasisi ya Sanaa na
Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Bw. Baraka Jeje (kushoto) alipotembelea banda lake kabla ya kufungua
Tamasha la 36 la Sanaa na Utamaduni la kimataifa Bagamoyo jana katika Taasisi
ya TaSUBa
Baadhi
ya wanafunzi kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) wakiimba
wimbo wa taifa wakati wa uzinduzi wa Tamasha la 36 la Sanaa na Utamaduni la kimataifa
Bagamoyo jana katika Taasisi hiyo.
Wanafunzi kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni
Bagamoyo (TaSUBa) wakicheza ngoma wakati wa uzinduzi wa Tamasha la 36 la Sanaa
na Utamaduni la kimataifa Bagamoyo jana katika Taasisi hiyo.
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (watatu
kulia) akishirikiana na Mtendaji Mkuu kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni
Bagamoyo Dkt. Herbert Makoye (wapili kulia), Katibu Tawala Wilaya ya Bagamoyo
Mhe. Erica Yegelea (watatu kushoto), Mtendaji Mkuu Baraza la Sanaa la Taifa
(BASATA) Bw. Godfrey Mngereza (kulia) na Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo Mhe.
Shukuru Kawambwa (wapili kushoto) kukata keki kuashiria uzinduzi wa Tamasha la
36 la Sanaa na Utamaduni la kimataifa Bagamoyo jana katika Taasisi ya TaSUBa.
Picha na: Genofeva Matemu - WHUSM
Na: Genofeva Matemu – WHUSM
Bodi ya Ushauri ya
Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) imeagizwa kukaa na kufanya
tathmini ya kina kuandaa mpango mkakati mzuri wa namna ya kuliendesha tamasha la
Sanaa na Utamaduni ili liweze kuwa na tija zaidi kwa wasanii na Taasisi kwa
ujumla.
Rai hiyo imetolewa na
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe wakati
wa uzinduzi wa tamasha la 36 la Sanaa na Utamaduni la kimataifa Bagamoyo jana
katika Taasisi hiyo mjini Bagomoyo.
“Tangu kuanzishwa kwa
tamasha hili mwaka 1982, Tamasha limeendelea kuwa kivutio kikubwa kwa wasanii
na wadau wa sanaa ndani na nje ya nchi na wananchi kwa ujumla hivyo ni vyema
Bodi ya ushauri ya TaSUBa ikapanga mikakati yenye tija zaidi kwa maslahi ya
wasanii wetu na Taasisi yetu” amesema Mhe. Mwakyembe.
Aidha Mhe. Mwakyembe
ameipongeza Bodi, Menejimenti, wafanyakazi na wanachuo wote wa TaSUBa kwa kazi
kubwa wanayoiofanya kila mwaka ya kuandaa na kuendesha Tamasha hilo kwa kipindi
cha miongo mitatu na nusu mfululizo na kuwataka kutembea kifua mbele kwa rekodi
hiyo iliyotukuka ndani na nje ya nchi.
Mhe. Mwakyembe amesema kuwa lengo la Tamasha hilo
ni pamoja na kutunza na kuenzi sanaa na utamaduni wa mtanzania, kutengeneza
jukwaa ambalo wanafunzi wa TaSUBa wanalitumia kupima kiwango chao cha umahiri
katika sanaa kwa mwaka, kukutanisha watu wa tamaduni mbalimbali kutoka sehemu
tofauti duniani ili kuonyesha utajiri wao wa sanaa na utamaduni, pamoja na
kutengeneza jukwaa ambalo ni kiungo cha kujenga mahusiano ya wasanii wa ndani
na nje ya nchi kupitia maonyesho ya sanaa na kubadilishana uzoefu na uwezo
katika kuendeleza tasnia ya sanaa.
Kwa upande wake
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Dkt. Herbert
Makoye amesema kuwa taasisi inajivunia mafanikio makubwa wanayoendelea kuyapata
kupitia tamasha hilo kwani kwa sasa tamasha linajumuhisha wasanii wa ndani na
nje ya nchi pamoja na wanafunzi waliosoma katika taasisi hiyo miaka ya nyuma na
waliopo mafunzoni.
Aidha Dkt. Makoye
amewashukuru wakazi wa Bagamoyo kwa ushirikiano ambao wamekua wakiuonyesha
katika kushirikiana na Taasisi kuendeleza na kuthamini sanaa na utamaduni wa
mtanzania.
Naye Chifu wa
Unyanyembe na Mwenyekiti wa Chama cha Machifu Tanzania Mhe. Msagati Fundikira
amewapongeza watendaji wa TaSUBa kwa kutoa wataalamu wazuri katika fani ya
sanaa na utamaduni kwani kwa ufanya hivyo wamekua wakiendeleza na kudumisha
utamaduni wa mtanzania kwa vizazi vya leo.
Tamasha hili la 36 la
Sanaa na Utamaduni la kimataifa la Bagamoyo lenye kauli mbiu isemayo “Sanaa na
Utamaduni katika kupiga vita madawa ya kulevya” limeshirikisha wasanii kutoka
Kenya, Ufaransa, Uingereza, Zimbabwe na Mayyote na kuudhuriwa na mabalozi
mbalimbali akiwemo balozi wa Malawi, balozi wa Palestina, balozi wa uholanzi,
pamoja na wawakilishi kutoka ubalozi wa Zambia, Saudi Arabia, Msumbiji, Japani,
Ujerumani, Marekani, India, Shirikisho la Urusi, Angola na Kenya.
No comments:
Post a Comment