Habari za Punde

Waziri wa Fedha na Mipango Tanzania Mhe. Dkt. Mpango Akagua na Kutoa Maagizo Kuhusu Madini ya Almasi Yaliokamatwa Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Filip Mpango (katikati) akiwa na viongozi wengine wa Serikali, Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP) Biswalo Mganga (kushoto), Kamishna Mkuu wa  Mamlaka ya Mapato nchini TRA Charles Kichere(kulia) wakiangalia Mzigo wa Almasi uliokamatwa katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Filip Mpango akisoma maelezo ya mzigo huo ambayo yalikuwa tofauti kabisa na uhalisia mara baada ya kuhakikiwa na timu ya  Wataalamu wa Kitanzania wazalendo.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Filip Mpango akiangalia Mzigo huo wa Almasi kutoka kwenye kampuni moja ya uchimbaji wa madini hayo Mwadui mkoani Shinyanga, mara baada ya kuhakikiwa na Wataalamu Wazalendo waligundua  kuwa mzigo huo una uzito Kg. 29 tofauti na Kg.13 zilizoanishwa na wahusika wa mzigo huo, na thamini yake ni zaidi ya Tsh. Bilioni 64.
Sehemu ya Mzigo huo wa Almasi uliokamatwa katika uwanja wa Ndege ambao thamani yake ni zaidi ya Tsh. Bilioni 64.

Profesa Abdulkarim Mruma akiwasilisha Taarifa yake ya Uchunguzi wa Madini yaliyokamatwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Picha na Mpiga Picha Maalum. 
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Filip Mpango akizungumza wakati akipokea Ripoti ya Uchunguzi wa Madini hayo ya Almasi jijini Dar es Salaam(Picha na Ikulu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.