Habari za Punde

KANGI LUGOLA AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Kangi Lugola (kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Faustine Kamuzora  (kulia) mara baada ya mazungumzo ambapo  Mhe. Kangi Lugola alijitambulisha  kwa mara ya kwanza kama Naibu wa Wizara hiyo kwa Makamu wa Rais.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Kangi Lugola (katikati)akitembea kwa miguu akielekea ofisini kwake barabara ya Luthuli mara baada ya kumaliza mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Faustine Kamuzora. (picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.