Habari za Punde

Miradi Mbalimbali Yazinduliwa Wakati wa Mbio za Mwenge Kisiwani Pemba.

KIONGOZI wa mbio za mwenge wa uhuru Amour Ahmad Amour, akimpa mtoto Radhiya Said Mussa tone la vitamin “A” mara baada ya kukifungua kituo cha afya daraja la pili cha Pujini wilaya ya Chakechake, mara baada ya kukifungua kituo hicho, ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za mwenge huo wilayanyani humo
KIONGOZI wa mbio za mwenge wa uhuru Amour Ahmad Amour (kushoto), akiwa katika zoezi la kugawa vyandarua wakati wa hafla ya shamrashamra za mbio za mwenge kisiwani Pemba, Afisa wa Afya wilaya ya Chakechake, Kombo Omar Abdalla (mwenye vyandarua)
MSOMA risala ya ujenzi wa nyumba bora, Harith Bakar Nassor, mbele ya kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Amour Ahmad Amour, kabla ya nyumba hiyo iliopo Matuleni kuiwekea jiwe la msingi, kwenye shamra shamra za mwenge huo wilaya ya Chakechake
NYUMBA ya familia Asumini Hamad Said, iliopo Matuleni wilaya ya Chakechake, ambayo jana imewekewa jiwe la msingi na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru, Amour Ahmad Amour, ikiwa ni sehemu ya shamra shamra ya mwenge huo, wilayni humo
KIONGOZI wa mbio za mwenge wa uhuru Amour Ahmad Amour, akiondoa kitambaa kuashiria kuiwekea jiwe la msingi, nyumba bora ya familia Asumini Hamad Said, iliopo Matuleni wilaya ya Chakechake, kwenye shamra shamra za mwenge huo wilayanyani humo
KIONGOZI wa mbio za mwenge wa uhuru Amour Ahmad Amour, akiondoa kitambaa kuashiria kukifungua kituo cha afya cha daraja la pili, kiliopo Pujini wilaya ya Chakechake,  kwenye shamra shamra za mwenge huo wilayani humo.
 (Picha na Haji Nassor, Pemba).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.