Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Issa Gavu (kulia)
akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari kuhusu tathimini ya ziara ya
Ujumbe wa Mfalme wa Oman, Qaboos bin Said Al-Said uliozuru Zanzibar hivi
karibuni. Kushoto ni Mshauri wa Rais wa Zanzibar katika masuala ya Ushirkiano
wa Kimataifa, Fedha na Uchumi Mohamed Abdiwawa.
Baadhi ya Waandishi wa vyombo vya habari wakifuatilia mkutano wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Issa Gavu (kulia) akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari kuhusu tathimini ya ziara ya Ujumbe wa Mfalme wa Oman, Qaboos bin Said Al-Said uliozuru Zanzibar hivi karibuni.
Baadhi ya Waandishi wa vyombo vya habari wakifuatilia mkutano wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Issa Gavu (kulia) akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari kuhusu tathimini ya ziara ya Ujumbe wa Mfalme wa Oman, Qaboos bin Said Al-Said uliozuru Zanzibar hivi karibuni.
Baadhi ya Waandishi wa vyombo vya habari wakifuatilia mkutano wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Issa Gavu (kulia) akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari kuhusu tathimini ya ziara ya Ujumbe wa Mfalme wa Oman, Qaboos bin Said Al-Said uliozuru Zanzibar hivi karibuni.
Na Ismail Ngayonga MAELEZO
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imetoa hofu
wananchi na kuwaeleza kuwa mataifa mbalimbali duniani yanaendelea kuunga mkono
na kutoa ushirikiano mkubwa kwa Rais Dkt. Ali Mohamed Shein katika jitihada
mbalimbali zake za kuwalelea maendeleo Wazanzibar.
Hayo
yamesemwa leo (Jumamosi Oktoba 21, 2017) Mjini Zanzibar na Waziri wa Nchi Ofisi
ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Issa Gavu wakati alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tathimni ya ziara ujumbe wa Mfalme wa
Oman, Qaboos bin Said Al-Said aliyetembelea Zanzibar tarehe 22 Septemba mwaka
huu.
Gavu
alisema katika kudhihirisha kuimarika kwa uhusiano na mataifa mbalimbali duniani,
Serikali ya Zanzbar tayari imepokea mialiko tisa ya ziara za nje ya nchi
zinazotarajiwa kufanywa na Rais Dkt. Ali Mohamed Shein na Viongozi wa
Serikali
kuanzia mwishoni mwa mwezi Januari 2018.
“Serikali
inaendelea kupanua wigo wa ushirikiano wa kidiplomasia na mataifa ya kigeni,
hakuna haja ya wananchi kuwa na hofu, na tutaendelea kukaribisha ushirikiano na
mataifa ya nchi jirani kwa ajili ya kuharakisha maendeleo ya wananchi wetu”
alisema Gavu
Gavu
alisema tangu kuingia madarakani kwa Rais Shein, Novemba 2015 uhusiano wa
Zanzibar na mataifa mbalimbali ulimwengu umekuwa ukiimarika na kueleza kuwa Kiongozi
tayari amesafiri katika mataifa ya Djibout, Morroco na Commoro.
Aidha
Gavu alisema katika kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia na nchi marafiki, nchi
ya Saudi Arabia inatarajia kufungua Ofisi ndogo ya Ubalozi Zanzibar na hivyo kuwataka
Wananchi wa Zanzibar kuendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali yao
ikiwemo kudumisha amani, umoja na mshikamano.
Akizungumzia
kuhusu ziara ya Mfalme Qaboos bin Said Al-Said wa Oman aliyoifanya Zanzibar hivi
karibuni, Serikali ya Zanzibar tayari imeunda timu ya wataalamu kwa ajili ya
kufuatilia utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa baina ya mfalme wa Oman na
Rais Shein.
Aliongeza
kuwa katika ziara hiyo, Mfalme wa Oman alikubali kutoa ufadhili wa mafunzo ya
muda mfupi na mrefu kwa wanafunzi wa wanafunzi wa Zanzibar katika masuala ya
mafuta na gesi pamoja na kujenga viwanda vya kusindika samaki.
“Tutahakikisha
kuwa tunapeleka vijana wenye sifa na weledi katika masomo hayo ili kuhakikisha
kuwa Zanzibar inatumia vyema fursa hiyo, ambapo kwa kuanzia hivi sasa wapo
wanafunzi wa masomo hayo katika nchi ya China wakipata ujuzi wa tasnia ya
mafuta” alisema Gavu.
Wakati wa ziara ya ujumbe wa Oman, Waziri Gavu alieleza
kuwa katika mazungumzo ya ya ujumbe huo na Rais Shein, Mfalme Qaboos bin Said
Al-Said alikubali pia kufanya matengenezo makubwa ya jengo la Beit –el Ajab
pamoja na jengo la “People’s palace”, hatua inayolenga kuimarisha ukuaji wa
sekta ya utalii Zanzibar.
Kwa upande wake Mshauri wa Rais wa Zanzibar katika
masuaala ya Ushirikiano wa Kimataifa, Fedha na Uchumi, Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa
aliwataka Wazanzibar kuungana pamoja na kuendelea kumuunga mkono Rais Ali
Mohamed Shein hususani katika jitihada zake za kuimarisha ushirikiano na
mataifa ya kigeni.
Balozi Ramia alisema katika siku za hivi karibuni
kumeibuka hofu isiyo na sababu kuhusu ziara ya Mfalme Qaboos Said Al-Said na
kueleza kuwa katika mazungumzo baina ya Viongozi hao wawili hakukuwa na suala la
kisiasa lililojadiliwa badala yake ni masuala ya uimarishaji wa ushirikiano wa
maendeleo ya wananchi.
“Kuna minong’ono kuwa Zanzibar ilibanwa na mfalme
Qaboos Said Al-Said kuhusu hali ya kisiasa, jambo hilo hakuna na badala yake
Viongozi ho walijadili masuala ya ushirikiano na hatua zinazopaswa kuchuliwa
ili kuharakisha maendeleo ya wananchi wa pande zote mbili”
No comments:
Post a Comment