Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein Azungumza na Ujumbe wa Benk ya CRDB Ikulu Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akipokea Hundi ya Shilingi za Kitanzania Millioni Ishirini na  kutoka kwa Mkurugenzi Masoko katika Benki ya CRDB Nd,Tully Esther Mwambapa,zilizoahidiwa na Benki hiyo kwa ajili ya mchango wa madawati kwa Skuli za Serikali, sambamba na kupokea Milioni tano kwa ajili ya Ujenzi katika  Skuli ya chekechea Madungu Wilaya ya Chakechake Pemba, ujumbe wa Benki hiyo ulipofika Ikulu Mjini Unguja leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza  na ujumbe wa Benki ya CRDB unaoongozwa na Mkurugenzi Masoko Nd,Tully Esther Mwambapa  (wa pili kulia) ulipofika Ikulu Mjini Unguja leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akifuatana na mgeni  wake Mkurugenzi Masoko wa Benki ya CRDB Nd,Tully Esther Mwambapa baada ya mazungumzo na Ujumbe wa Benki hiyo ulipofika Ikulu Mjini Unguja leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiagana  na Mkurugenzi Masoko wa Benki ya CRDB Nd,Tully Esther Mwambapa baada ya mazungumzo alipofika Ikulu Mjini Unguja leo akiwa na Ujumbe aliofuatana nao, [Picha na Ikulu.] 09 /11/2017.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.