Habari za Punde

Tangazo la nafasi za kazi Wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira
Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi kwa ajili ya Wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira kama ifuatavyo:-

1. Petroleum Engineer Daraja la II “Nafasi 2”
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza ya Petroleum Engineer kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

2. Oil and Gas Well Engineer Daraja la II “Nafasi 1”
Sifa za muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza inayohusiana na Masuala ya Well Engineering au inayofanana na hiyo kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

3. Geologist Daraja la II “Nafasi 1”
Sifa za muombaji:

• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza inayohusiana na 
Masuala ya Geology au inayofanana na hiyo kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

4. Mining Engineer Daraja la II “Nafasi 1”
Sifa za muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya ‘Madini’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

5. Karani Masjala Daraja la III “Nafasi 1”
Sifa za muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Record Management kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

6. Msaidizi ICT Daraja la III “Nafasi 1”
Sifa za muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada katika fani ya ICT kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.


7. Energy Development Engineer Daraja la II “Nafasi 1”
Sifa za muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza ya Electronics Engineer kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Jinsi ya Kuomba:
• Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU,
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 - ZANZIBAR.

• Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. 

Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 10 Novemba. 2017 wakati wa saa za kazi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.