Kamishna
wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu (kati kati), akiwatoa hofu Watendaji
wa Mamalaka ya Vitambulisho vya TAifa (NIDA) kwamba kuanzia mwezi January 2018,
Idara ya Uhamiaji Zanzbar imejipanga kushughulikia maombi ya Vitambulisho vya
Taifa kwa Raia wote watakaofika katika Ofisi yao iliyopo Kinduni, Wilaya ya
Kaskazini “B” Unguja, badala ya kufuata huduma Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa
Kaskazini iliyopo Kivunge. Hatua hiyo ni utekelezaji wa Ahadi za Serikali
kufikisha huduma karibu na Wananchi. Aliyasema hayo wakati alipotembelea Ofisi
hizo wakati wa ziara ya kikazi katika Wilayani humo tarehe 05 - 06 Disemba, 2017.
Sheha wa Shehia ya Kiwengwa Bwana Maulid Masoud Ame, akimuleza Kamishna
wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu na Maafisa waandamizi wa Idara hiyo
alioambatana, changamoto za wageni katika maeneo yao. Wakat wa ziara ya kikazi kujionea
utendaji kazi wa Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Unguja na Wilaya zake tarehe
05 - 06 Disemba, 2017.
Kamishna
wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu (kati kati), akielezea jinsi Idara
ya Uhamiaji inavyopiga hatua katika kutatua changamoto ya ufinyu wa Ofisi na
Vitendea kazi katika Wilaya zote Unguja na Pemba, ambapo alisema hivi karibuni
Idara yake inatarajia kupokea magari (12) na Pikipiki (20) ambazo kwa kiasi
kikubwa zitakidhi uhaba uliopo. Aliyasema hayo wakati wa ziara ya kikazi kwenye
maeneo mbali mbali Mkoa wa Kaskazini Unguja tarehe 05 - 06 Disemba, 2017.
Kamishna
wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu, akiambatana na Maafisa Waandamizi
wa Uhamiaji wakitembelea maeneo mbalimbali yanayotumiwa na Wahamiaji wasiofata
Sheria katika ukanda wa Pwani za Kiwengwa, Pwani mchangani, Matemwe, Pongwe,
Kendwa na Nungwi, wakati alipofanya ziara ya kikazi katika maeneo yote yanayofanyiwa
kazi na Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Unguja tarehe 05 - 06 Disemba, 2017.
Mkaguzi
Msaidizi wa Uhamiaji, Haroub Iddi Juma, akitoa ufafanuzi kwa Kamishna wa
Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu juu ya Ramani ya Kiwanja kilichopo
kijiji cha Gamba, Wilayani ya Kaskazini “B” wakati alipotembelea kiwanja hicho jana
tarehe 05 Disemba, 2017 kinachotarajiwa kujengwa Ofisi ya Uhamiaji Wilayani
humo.
Sheha
wa Shehia ya Moga Bwana Juma Kombo Juma (kati kati), akimuonesha Kamishna wa
Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu mipaka ya Kiwanja kilichopo Shehia ya
Gamba, Wilaya ya Kaskazini “B” kinachomilikiwa na Idara ya Uhamiaji. Hizo ni
juhudi za Idara hiyo kufikisha huduma zake karibu na wananchi kwa kujenga Ofisi
na Makaazi ya Askari katika Ofisi za Mikoa na Wilaya zote zilizopo Zanzibar.
No comments:
Post a Comment