Habari za Punde

Na. Othman Khamis OMPR.

Rais wa Zanzibar Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Muhamed Shein amesema Kiwango duni cha uwajibikaji katika misingi ya kuendesha Utawala Bora Kisiasa na Kiuchumi miongoni mwa Nchi za Bara la Afrika kimekuwa kikichangia na kusababisha migogoro isiyokwisha ambayo huwaathiri Wananchi walio wengi ndani ya eneo kubwa la Bara hilo.

Amesema hicho ni moja ya kitu hatari kinachosababisha kuporomoka kwa Uchumi, Maendeleo na Ustawi wa Jamii Barani Afrika changamoto inayopaswa kutoa  fursa kwa Waafrika wenyewe kutafakati kwa kina njia gani yenye muelekeo wa mafanikio katika masuala ya kufanikisha Maendeleo na Utawala Bora.

Othman Khamis kutoka Arusha anatupa Taarifa zaidi...mwisho. Dr. Ali Muhamed Shein amesema hayo katika Hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  wakati alipokuwa akiufungua Mkutano wa 47 wa Kimataifa  wa kuwaandaa Watafiti Chipukizi wa Bara la Afrika katika dhana nzima ya kusaidia mataifa yao
Kitaaluma uliofanyika katika Hoteli ya Kimataifa ya Maunt Meru Mkoani Arusha.

Amesema Mataifa mengi Barani Afrika yamekuwa na ongezeko kubwa la idadi ya Watu hasa Vijana kasi ambayo inahitaji nguvu kubwa zitakazozaa  maarifa za Kiutafiti  katika masuala ya Uchumi ili  itoe afueni ya Maendeleo ya muelekeo wa matumaini.

Alisema uwajibikaji wa pamoja katika  umuhimu wa kuandaa nguvu za kiutendaji kwa kuwashirikisha Wananchi na hasa Vijana wenye Vipaji vya Utafiti wa kawaida ndani ya Taasisi za Kitaaluma unaweza kuzinyanyua Kiuchumi Nchi za Afrika katika kipindi kifupi.

Mapema Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi Afrika {AERC } Prosefa Lemma Senbet alisema Watafiti wa Taasisi hiyo wamekuwa wakifanya utafiti kwa kushirikiana na Taasisi nyengine ya Kimataifa takriban kwa Miaka 30 sasa.

Profes lemma alisema ushirikiano huo kwa kiasi kikubwa umesaidia kuibua Watafiti Chipukizi Barani Afrika ambao kwa sasa wamekuwa chachu ya muelekeo wa Matumaini kwa Mataifa wanayotoka.

Alisema katika dhana nzima ya nguvu za uwajibikaji katika sekta ya Utafiti AERC imeweka utartibu maalum wa kuwatumia Wataalamu mbali mbali waqzoefu waliobobea katika fani hiyo ili kusaidi maarifa yanayoweza kuongeza nguvu na kasi ya uvumbuzi hasa katika masuala ya Kiuchumi.

Akimkaribisha Mgeni rasmi kuufungua Mkutano huo wa 47 wa Kimataifa  wa kuwaandaa Watafiti Chipukizi wa Bara la Afrika Gavana wa Benki  Kuu ya Tanzania { BOT } Profesa BennoNdulu  alisema kinachohitajika kwa Watu wa Afrika wakati huu ni kuangalia muelekeo wa namna gani Mataifa ya Bara la Afrika yanavyojikita katika uimarishaji wa uchumi kwa
kuzingatia Utawala Bora.

Profesa Benno alisema kutokana na mabadiliko ya Dunia yanayokwenda kwa kasi kupitia mfumo wa kisasa wa Teknolojia ya Mawasiliano, Jamii za Waafrika wanalazimika kubadilika kwa haraka ili waende na wakati huo.

Alitahadharisha kwamba  changamoto za Rushwa, migomo ya mara kwa mara , uhabawa vyombo vya usafiri zinazooneka kuzielemea Nchi za Bara la Afrika iwapo hazikutizamwa na kuchukuliwa  hatua zinazofaa zinaweza kuviza maendeleo ndani ya Nchi za Bara la Afrika.

Mkutano huo unaofanyika kila baada ya Miaka Miwili katika Mataifa Wanachama huandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi Afrika { AERC } kwa lengo la kuwandaa Vijana waenye vipaji katika masuala ya Tafiti mbali mbali zikiwemo Uchumi, Kilimo, Uhandisi  na Afya.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.