Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, Ashiriki katika Mazishi ya Marehemu Bi. Mtumwa Mgeni leo.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Waumini wa Dini ya Kiislam wakishiriki katika Sala ya kuuombea mwili wa Marehemu Mtumwa Mgeni Mama Mzazi wa Meja Mstaaf Juma Kassim Tindwa , Sala iliyokuwa ikiongozwa na Sheikh Nomani Jongoo katika msikiti wa Kilimani na kuzikwa katika makaburi ya kwarara nje kidogo ya mji wa Unguja.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiweka mchanga katika kaburi la marehemu Mtumwa Mgeni, wakati wa mazishi yake yaliofanyika katika makaburi ya Kijiji kwao Kwarara Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
 Sheikh Sharif Abdurahaman akisoma dua katika kaburi la marehemu Mtumwa Mgeni baada ya mazishi yake yaliofanyika katika makaburi ya Kwarara Nje Kidogo ya Mji wa Zanzibar leo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.