Habari za Punde

Rais Shein, Ajumuika na Wananchi wa Zanzibar Katika Mazishi ya Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi Serikali Marehemu Othman Bakari leo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Aki Iddi wakijumuika na Wananchi wa Zanzibar katika ibada ya Sala ya kuuombea mwili wa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi Serikali Zanzibar Marehemu Othman Bakari ukisaliwa katika Masjid Shurba sala hiyo ikiongozwa na Sheikh Fadhil Soraga, marehemu amezikwa katika makaburi ya mwanakwerekwe Zanzibar na kuhudhuriwa na Viongozi wa Serikali na Chama.na Wananchi mbalimbali. 
Waumini wa Kiislamu wakishiriki katika Sala ya kuusalia mwili wa Marehemu Othman Bakari, aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi Seriali, aliyefari jana na kuzikwa leo katika makaburi ya mwanakwerekwe Zanzibar.  


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.