Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Ajumuika na Wananchi Katika Taraab Rasmin ya Kusherehekea Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar . Katika Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud alipowasili katika viwanja vya zamani vya Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Zanzibar kuhudhuria hafla ya Taarab rasmin ya kusherehekea Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar uiliotumbuizwa na Kikundi cha Taifa cha Taarab Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe. Rashid Juma Ali alipowasili katika viwanja vya Zamani vya Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Zanzibar kuhudhuria hafla ya Taarab.
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo Omar Hassan King. alipowasili katika viwanja vya zamani vya ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Zanzibar kuhudhuria hafla ya Taraab rasmin ya kusherehekea Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mama Fatma Karume na Mama Asha Suleiman wakati akiwa katika ukumbi wa hafla ya Taarab rasim ya Kikundi cha Taifa cha Taraab Zanzibar. 
Kikundi cha Taifa cha Taraab Zanzibar kikipiga Wimbo wa Taifa kabla ya kuaza kwa hafla hiyo ya kutowa burudani wakati wa kuadhimisha Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar  yanayoadhimishwa kila mwaka ifikapo 12 January.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, kulia Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na kushoto Waziri wa Habari Utalii Utamadni na Michezo Mhe. Rashid Ali Juma, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud wakiwa wamesimama wakat ukipigwa Wimbo wa Taifa kabla ya kuaza kwa hafla hiyo.
Wasanii wa Kikundi cha Taifa cha Taraab Zanzibar kikutoa burudani ya muziki wa Alam tupu kabla kuaza kwa burudani hiyo, iliofanyika katika ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Zanzibar. 











 


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.