Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Atembelea Mradi wa Kiwanda Cha Kusafishia Mafuta Katika Eneo la Mangapwani Unguja.

Baadhi ya Matanki katika Kiwanda cha Kusafisha Mafunta kinachojengwa katika eneo la Mangapwani Zanzibar na Wawekezaji Wazaliwa na kitotoa huduma ya kupokea mafuta kutoka moja kwa moja Uarabu na kuyasafisha kwa kupata aina mbalimbali ya mafuta ya Petroli, Dezeli na Mafuta ya Taa na mengineyo bila ya kuleta athari za kimazingira. Na kutoa Ajira kwa Wazanzibar wengi.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Salama Intarnational trading Co. Ltd Abdallah Said Abdallah, akitowa maelezo ya mradi wao wa Ujenzi wa Kiwanda cha kusafishia Mafuta ya Petroli kinachoendelea na ujenzi wake katika eneo la Mangapowani Mkoa wa Kaskazini Unguja wakati wa ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, alipotembelea eneo lililotengwa kwa ajili ya Ujenzi wa Matenki ya kuhifadhia Mafuta katika eneo la Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akizungumza wakati wa ziara yake kutembelea eneo lililotengwa kwa ajili ya Mradi wa Ujenzi wa kuhifadhia Mafuta katika ukanda wa Mangapwani Zanzibar, kulia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.