Habari za Punde

Ubalozi wa Denmark waandaa mkutano kujadili fursa za uwekezaji kwenye nishati ya umeme wa Upepo

Kampuni ya Vestas A/S ya Denmark kwa kushirikiana na Ubalozi wa Denmark nchini kwa mwongozo wa Wizara ya Nishati wameandaa mkutano wa kujadili fursa za uwekezaji katika nishati ya upepo (wind energy) nchini.
Mkutano huo ambao umewakutanisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi ukiwa na lengo la kujadili na kuibua fursa muhimu za nishati ya upepo ili kuongeza upatikanaji wa umeme wa uhakika nchini, umefunguliwa na Kaimu Kamishna wa Nishati na Masula ya Petroli, Mhandisi Innocent Luoga kwa niaba ya Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani.
Balozi wa Denmark Nchini Tanzania, Einar Hebogard Jensen akitoa maelezo juu ya mkutano wa wadau wa nishati ya upepo ulioandaliwa na kampuni ya nishati ya Vestas A/S kutoka Denmark kwa kushirikiana na Ubalozi wa Denmark nchini Tanzania.
Kaimu Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli, Mhandisi Innocent Luoga akisoma risala na kufungua mkutano wa wadau wa nishati ya upepo kwa niaba ya Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi wa kampuni ya Vestas A/S kwa Afrika Kusini, akielezea mipango ya kampuni hiyo ya kuwekeza kwenye umeme wa upepo nchini Tanzania.

Meya wa Manispaa ya Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe akitoa maelezo kuhusiana na fursa za uwekezaji wa umeme wa upepo katika mkoa wa Dodoma wakati wa mkutano wa wadau wa nishati ya upepo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Windlab Africa, Peter Venn akitoa mada wakati wa mkutano huo
Mkurugenzi wa Mradi wa Aldwych International, Mark Gammons akiwasilisha mada kuhusu miradi inayofanyika nchini Tanzania ikiwemo mradi wa umeme wa upepo  wa Singida wenye Megawati 100 na Ruhudji  wenye Megawati 358 wakati wa mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali wa masuala ya nishati wa ndani na nje ya Tanzania.
Baadhi ya wadau wakifuatilia mada kwenye mkutano huo wenye lengo la kujadili namna ya kuwekeza kwenye nishati ya Umeme wa Upepo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.