JENGO la Skuli ya Madungu Sekondari Pemba, ambalo
lilijengwa kwa msaada wa fedha za Benk ya Dunia na kufunguliwa na Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Mhe:Dk Ali Mohamed Shein, Januari
mwaka 2013 jengo hilo kwa sasa limekuwa linavuja kipindi cha mvua huku
wanafunzi wakishindwa kusoma.(PICHA NA
ABDI SULEIMAN, PEMBA)
WAJUMBE wa Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi
Zanzibar, wakiwa na viongozi wa Wizara ya Elimu Zanzibar, wakiwasikiliza
wanafunzi waliomo ndani ya moja ya madarasa yanayovuja kipindi cha mvua, huku
wanafunzi wakishindwa kusoma wakati wajumbe hao waliotembelea skuli hiyo na
kujionea athari zilizopo.(PICHA NA ABDI
SULEIMAN, PEMBA)
WAJUMBE wa Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi
Zanzibar, wakiangalia juu katika moja ya madarasa pamoja na watendaji wa Wizara
ya Elimu Zanzibar, wakiongozwa na ktibu mkuu wa Wizara hiyo Khadija Bakari
Juma, wakati wajumbe hao walipotembelea skuli hiyo na kuangalia athari zilizopo.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MJUMBE wa kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi
Zanzibar na Mwakilishi wa jimbo la Tunguu, Mhe:Simai Mohamed Said, akimuuliza
jambo katibu mkuu Wizara ya ELimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Khadija Bakari
Waziri wakati alipotembelea skuli ya Madungu Sekondari na kujionea athari
zilizopatikana kutokana na skuli hiyo kuvuja kipindi cha Mvua.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MOJA ya sehemu ya juu ya darasa la skuli ya Madungu
Sekondari, ikiwa imeharibika baada ya sehemu ya paa la skuli hiyo kuvuja katika
kipindi cha mvua, maji kuharibu silingbord yote ya darasa hilo kama
linavyoonekana katika picha.(PICHA NA
ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MAKAMU mwenyekiti wa kamati ya bajeti ya baraza la
Wawakilishi Zanzibar, mwakilishi wa jimbo la Chambani Bahati Khamis Kombo
akiongoza kikao cha wajumbe wa kamati yake na viongozi wa Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Amali Zanzibar, huko katika ukumbi wa skuli ya Madungu Sekondari Mjini
Chake Chake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN,
PEMBA)
WAJUMBE wa kamati ya bajeti ya baraza la Wawakilishi
Zanzibar, wakitoka kukagua skuli ya Dk Omar Ali Juma Wawi Chake Chake Pemba,
ikiwa ni moja ya skuli zilizoathiriwa na mvua kubwa ilionyesha Zanzibar.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Khadija Bakari Juma akisoma taafira ya mradi wa ZABEIP, kwa wajumbe wa kamati ya bajeti ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, wakati walipotembelea jengo la skuli ya Madungu Sekondari Chake Chake Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
No comments:
Post a Comment