Habari za Punde

Balozi Seif akutana na Mabalozi wapya walioteuliwa karibuni

 Balozi wa Tanzania Nchini Sweeden Dr. Wilbrod Slaa Kushoto akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipofika yeye na Mwenzake Balozi Muhidin Ali Mboweto anayekwenda Nigeria walipofika kuaga rasmi. Kati kati yao ni Balozi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Nigeria  Muhidin Ali Mboweto.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kati kati akizungumza na Balozi wa Tanzania Nchini Nigeria Balozi Muhidin Ali Mboweto Kushoto na Balozi wa Tanzania Nchini Sweden Dr. Wilbrod Slaa Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Dr. SlaaKulia na Balozi Seif Kulia wakifanyiana mzaha walipokuwa wakikumbushana utumishi wao wakati walipokuwa Wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya M,uungano wa Tanzania mara baada ya mazungumzo yao.

Na Othman Khamis , OMPR


 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  alikutana kwa mazungumzo na Mabalozi  Muhidin Ali Mboweto  anayeiwakilisha Tanzania Nchini Nigeria na Dr. Wilbrod Slaa anayekwenda Nchini Sweeden walipofika Ofisini kwake kumuaga rasmi wakielekea katika vituo vyao vya kazi walivyopangiwa.
Katika mazungumzo yao Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwaeleza Mabalozi hao kwamba nafasi ya Ubalozi ni fursa nzito ya Uwakilishi wa Nchi inayopaswa kutumikiwa kwa uzalendo wa hali ya juu.
Balozi Seif  aliwaeleza Mabalozi hao wa Tanzania kwamba Nigeria na Sweeden ni Nchi zenye Historia kubwa ya ushirikiano na Tanzania inayopaswa wasimamizi hao wa Diplomasia kuangalia maeneo ambayo yanaweza kuendelea kudumisha Uhusiano huo.
Alisema zipo sekta ambazo Nigeria na Sweeden zinaweza kuisaidia Zanzibar Kitaaluma akitolea Mfano eneo la Utalii, Umeme Mbadala na hata masuala ya Uhifadhi wa Nyaraka kwa vile Mataifa hayo tayari yameshapiga hatua kubwa Kitaaluma.
Mapema Balozi wa Tananzania Nchini Sweeden Dr. Wilbrod Slaa kwa niaba ya mwenzake Balozi Muhidin Ali Mboweto anayekwenda Nigeria alisema wanajitambua kwamba wao  ni Wawakilishi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Dr. Slaa alimueleza Balozi Seif kwamba utumishi wao wa Kidiplomasia watauelekeza zaidi katika Diplomasia ya Kiuchumi kama Dunia ilivyobadilika kujikiota zaidi katika eneo hilo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.