Habari za Punde

Hali ya upatikanaji mafuta Zanzibar

Kaimu Mkurugenzi Huduma kwa Wateja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) Mussa Ramadhan Haji akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu hali ya Mafuta Zanzibar (Picha  na Kijakazi Abdalla Maelezo)

Na Kijakazi Abdalla,  Maelezo    

Hali ya Upatikanaji wa mafuta utaendelea kuwa wa kawaida  baada ya meli ya United Sprit 1 iliyokuwa imechukuwa mafuta kuanza kushusha na kusambazwa vituoni tekea jana .
Akizungumza na Waandishi wa habari huko katika Ofisi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) Kaimu Mkurugenzi Huduma kwa wateja Mussa Ramadhani Haji .
Amesema kuwa hali iliyojitokeza ya upungufu wa mafuta kwa takribani wiki mbili zilizopita hasa katika vituo vinavyomilikiwa na United Petroleum (UP) inatokana na meli ya kampuni ya United Petroleum kuwa ilikuwa katika foleni ya kusubiri kupakia mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam.
Aidha amesema kuwa Meli ya MT  Ukombozi ya Kampuni ya GAPCO nayo imefanikiwa kupakia mafuta ya Petroli na Dizeli jana jioni katika Bandari ya Dar es Salaam na imefika Zanzibar jana  na mafuta na kushushwa na kusambazwa vituoni leo.
Hata hivyo Kaimu Mkurugenzi huyo alisema kuwa Zura itaendelea kusimamia zoezi la usambazaji  na uuzwaji wa mafuta vituoni kwa kufuata taratibu za mamlaka.
Vilevile aliwaomba wananchi kuendeleza ushirikiano ili kuimarisha huduma za  nishati nchini na kuhakikisha kuwa hakuna changamoto yoyote katika upatikanaji wa mafuta nchini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.