Habari za Punde

Mawakili wa Serikali Watowa Elimu ya Sheria Kwa Wananchi Zanzibar.

Wakili wa Serikali Hamisa Mmanga Makame akitoa elimu kwa Wananchi kwa Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja  juu ya kupiga Vita udhalilishaji na Migogoro ya Ardhi katika Shehiya zao.
Mawakili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakitoa Elimu kwa Wananchi wa Mkowa wa Kaskazini Unguja  ili  kuifahamu vyema Sheria ya Mahakama ya Kadhi na Sheria ya Ardhi  na kupiga vita vitendi vya Udhalilishaji.
Mmoja ya Mawakili  Ali Issa Abdalla kitoa ufafanuzi kuhusu Sheria ya ardhi kwa Wananchi i wa Mkoa wa Kaskazini Unguja .
 Mwananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Yussuf Khalfan Haji akiuliza suali kwa Mawakili hao  juu ya migogoro ya Ardhi iliyopo katika shehiya yao .
Masheha wa Shehiya za Mkoa wa Kaskazini Unguja wakishiriki katika Elimu inayotolewa na Mawakili wa Serikali juu ya kupiga Vita udhalilishaji na Migogoro ya Ardhi katika Shehiya zao.  Picha na Miza Othman – Habari Maelezo- Zanzibar.
IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.
Na Miza Othman – Maelezo Zanzibar.       12/02/2018.
Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja wamewataka Mawakili kufanya kazi kwa uwadilifu katika kupunguza migogoro yanayowakabili wananchi katika shehiya zao.
Hayo wameyaeleza wananchi hao  huko Chuo cha Amali Mkokotoni wakati walipokuwa wakipatiwa Elimu ya Sheria ya Ardhi na kupiga vita aina zote za udhalilishaji zilizopo katika shehiya zao.
 Wanachi hao wamesema wamechoshwa na vitendo na vitendo vya udhalilishaji na migogoro ya Ardhi ambayo hujitokeza sikuhadisiku katika shehiya zao jambo ambalo linarudisha nyuma kimaendeleo.
Aidha wamesema ni vyema Mawakili hao kuwa mstari wa mbele katika kusimamia sheria za Wananchi hao ili kuhakikisha vitendo hivyo vinaondoka Nchini.
“Tumechishwa na vitendo hivyo simamieni Sheria tuondowe kabisa katika nchi yetu”,Walisisitiza  Wananchi hao.
 Nao Mawakili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  wamesema wataendelea kutoa elimu kwa Wananchi mbali mbali wa Vijijini ili kuzifahamu na kuzitekeleza vyema Sheria hizo.
Hata hivyo Mawakili hao wamewataka Wananchi hao  kuzifahamu ipasavyo  Sheria ya Ardhi na Sheria ya Mahakama ya Kadhi ili kuwawezesha  kuepukana na migogoro isiyokuwa ya lazima katika kutekeleza majukumu yao.
Aidha wamesema  wameamuwa  kupita maeneo ya vijijini kwa lengo la kuwapatia elimu wananchi  hao katika kumiliki Ardhi kisheria na kupiga vita aina zote za udhalilishaji zilizopo katika shehiya zao.
Mawakili hao wamesema kutokana  na sheria zilizowekwa  katika Mahkama hiyo Mtu yeyote atakae miliki Ardhi ni vyema kujisajili ili kuepuka migogoro isiyokuwa ya lazima ndani ya Serikali na jamii kwa ujumla.
Ali Issa Abdalla mmoja ya Mawakili alisema wamechoshwa na vitendo vya udhalilishaji wanavyovisikia siku hadi siku vikiendelea ndani ya jamii jambo ambalo linalowaumiza vichwa katika utekelezaji wamajukumu yao.
Alisema licha ya Vitendo hivyo kuripotiwa siku hadi siku lakini wananchi walio wengi bado hawajawa na utayari wa kwenda kutoa ushahidi mahakamani kama inavyotakiwa.
“Utafiti ulibainisha ya kwamba Sheria iliyofutwa ilikuwa na mapungufu kadhaa ambayo bila ya kuondolewa udhalilishaji wa kijinsia ungelibakia kupigiwa kelele za bure na utekelezaji wa haki katika Mahakama za Kadhi ungeendelea kusuwasuwa” Alisema Wakili huyo.
Hata hivyo amewataka wazazi na walezi kuwa karibu na Watoto wao na kufuatilia nyenendo zao ili kuondokana na matatizo yanayowakabili  watoto hao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.