Habari za Punde

MKUTANO WA WAJUMBE WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WAFANYIKA ZANZIBAR.

Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Kiswahili ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Pro,Kenneth Inyani Simala akizungumza na Wajumbe wa Bunge la Afrika mashariki waliofika Zanzibar kwa lengo la Kuimarisha Matumizi ya kiswahili katika Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Mkutano ul;iofanyika katika ukumbi wa Eakrotanal maisara mjini Unguja.
Mjumbe wa Bunge la Afrika mashariki Wanjiku Muhia akizungumza na  Wajumbe wa Bunge la Afrika mashariki waliofika Zanzibar kwa lengo la Kuimarisha Matumizi ya kiswahili katika Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Mkutano ul;iofanyika katika ukumbi wa Eakrotanal maisara mjini Unguja.
Baadhi ya Wajumbe wa Bunge la Afrika mashariki   waliofika Zanzibar kwa lengo la Kuimarisha Matumizi ya kiswahili katika Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Mkutano ul;iofanyika katika ukumbi wa Eakrotanal maisara mjini Unguja.
Mbunge wa Bunge la Jumuia ya Afrika mashariki Mariam Usi Yahya akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada kumaliza mkutano wa  Wajumbe wa Bunge la Afrika mashariki waliofika Zanzibar kwa lengo la Kuimarisha Matumizi ya kiswahili katika Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Mkutano ul;iofanyika katika ukumbi wa Eakrotanal maisara mjini Unguja.
Wajumbe wa Bunge la Afrika mashariki wakiwa katika Picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kwa Mkutano wenye lengo la   Kuimarisha Matumizi ya kiswahili katika Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Mkutano ul;iofanyika katika ukumbi wa Eakrotanal maisara mjini Unguja.

Na Miza Kona - Maelezo Zanzibar.      12/02/2018

Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) limesema linakusudia kukuza kiswahili na kuacha kutumia lugha za kikoloni ili iweze kutumika lugha kitaifa
 
Akizungumza na waandishi wa habari Mjumbe wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Wanjiku Muhia huko Kamisheni ya Kiswahili Zanzibar iliopo Eakrotanal alisema lugha ya kiswahili itumike kuwa lugha ya Taifa na kuitangaza kimataifa kwa lengo la kuikukuza lugha hiyo.

Alisema lugha Kamisheni ya Kiswahili ina lengo la kuratibu na kuhimiza Maendeleo na Matumizi ya kiswahili kwa ajili ya mawasiliano kikanda na kimataifa katika masuala ya kisiasa, kiuchumi, kisayansi na kiteknolojia kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

"Tunataka kiswahili kitumike kitaifa kwa nchi wananchama itumike kaika sehemu zote ikiwemo skuli, vyuoni na sehemu ambazo tunatumia lugha za kigeni ambapo itasaidia wananchi kuifahamu yale ambayo yanazunguzwa kwa lugha ya kiingereza"', alieleza Mjumbe huyo.

Alifahamisha kuwa kamisheni ya Kiswahili imekubaliana kuwa nchi wanachama kutumia lugha ya Kiswahili katika shughuli zote za kitaifa ili kuweza kukikuza na kuwanufaisha wasioweza kuitumia lugha hiyo.

Akizungumzia kuhusu changamoto zinaikalbili Kamisheni hiyo Mjumbe huyo alieleza kuwa ni uhaba wa fedha unaopelekea kutofikia malengo yaliyowekwa na Kamisheni hiyo.

Nae Maryam Ussi Yahya ambae pia ni Mjumbe wa Bunge hilo alisema Zanzibar ni kitovu cha kiswahili hivyo amewataka wananchi kuitumia vyema lugha hiyo kwa lengo la kukikuza na kueneza kwa wananchi wanaotaka kujifuanza.

Amefahamisha kuwa kamisheni inatarajia kutoa walimu watakaofundisha Kiswahili katika nchi Wanachama ambao hawafahamu vizuri lugha hiyo na kuweza kuzungumza kiswahili ili kutumike kwa ufasaha katika nchi hizo. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.