Habari za Punde

Msanii Maarufu Tanzania Diamond Akabidhi Hati za Kuanzisha TVna Redio Wasafi Zanzibar.

Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe. Rashid Ali Juma akimkabidhi hati ya Usajili ya Vituo vya Redio na TV ya Wasafii kwa Msanii Maarufu wa Muziki wa Bongo Flava Tanzania Diamond baada ya kukamilisha masharti ya usajili, hafla hiyo ya kukabidhi hati hizo umefanyika katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Zanzibar.  
Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe.Rashid Ali Juma akimkabidhi Hati ya  Usajili wa Kituo cha Redio ya Wasafi Msanii Maarufu wa Bongo Flava Diamond, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa zamani wa baraza la wawakilishi kikwajuni Zanzibar.
Msanii wa Bongo Flava Tanzania Diamond akionesha Hati za Usajili wa Vituo vya Redia na TV ya Wasafi Zanzibar.
Msanii wa Muziki wa Bongo Flava Tanzania Diamond akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa Hati za Usajili wa Vituo vyake vya Redio na TV na Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe. Rashid Juma Ali. hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa zamani kikwajuni.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.