Habari za Punde

Rais Dk Shein afanya mabadiliko madogo katika baraza la Mawaziri, aongeza Wizara moja

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amafanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mapinduzi kwa kuongeza Wizara moja zaidi, na kuwabadilisha Wizara baadhi ya Mawaziri. 

Kufuatia mabadiliko hayo, shughuli za Vijana zimehamishiwa katika Wizara mpya ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo; shughuli za Mazingira zimehamishiwa katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais; na shughli za Wakala wa Serikali wa Uchapaji zimehamishiwa Wizara mpya ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale. 

Aidha, amewateua Naibu Mawaziri wapya wawili na kumbadilisha Wizara Naibu Waziri mmoja. Kufuatia mabadiliko hayo, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hivi sasa itakuwa na Wizara 14 zenye Mawaziri na Naibu Mawaziri kama ifuatavyo:

1. OFISI YA RAIS NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI

i. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi- Mheshimiwa Issa Haji Ussi Gavu

2. OFISI YA RAIS, KATIBA SHERIA, UTUMISHI WA UMMA NAUTAWALA BORA

i. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora – Mheshimiwa Haroun Ali Suleiman

ii. Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora – Mheshimiwa Khamis Juma Mwalim





3. OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA SERIKALI ZA MITAA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

i. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ – Mheshimiwa Haji Omar Kheri

ii. Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ – Mheshimiwa Shamata Shaame Khamis


4. OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS

i. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais – Mheshimiwa Mohamed Aboud Mohamed

ii. Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais – Mheshimiwa Mihayo Juma Nhunga

5. WIZARA YA AFYA

i. Waziri wa Afya- Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed

ii. Naibu Waziri wa Afya – Mheshimiwa Harusi Said Suleiman

6. WIZARA YA ARDHI, NYUMBA, MAJI NA NISHATI

i. Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati – Mheshimiwa Salama Aboud Talib

ii. Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati – Mheshimiwa Juma Makungu Juma



7. WIZARA YA BIASHARA NA VIWANDA

i. Waziri wa Biashara na Viwanda – Mheshimiwa Balozi Amina Salim Ali

ii. Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda – Mheshimiwa Hassan Khamis Hafidh

8. WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI

i. Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali – Mheshimiwa Riziki Pembe Juma

ii. Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amal Mheshimiwa Mmanga Mjengo Mjawiri

9. WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

i. Waziri wa Fedha na Mipango – Mheshimiwa Dkt. Khalid Salum Mohamed

10. WIZARA YA HABARI, UTALII NA MAMBO YA KALE

i. Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale  - Mheshimiwa Mahmoud Thabit Kombo

ii. Naibu Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale – Mheshimiwa Choum Kombo Khamis


11. WIZARA YA KAZI, UWEZESHAJI, WAZEE, WANAWAKE NA WATOTO

i. Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto – Mheshimiwa Maudline Cyrus Castico

ii. Naibu Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto – Mheshimiwa Shadia Mohamed Suleiman

12. WIZARA YA KILIMO, MALIASILI, MIFUGO NA UVUVI

i. Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi – Mheshimiwa Rashid Ali Juma

ii. Naibu Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi – Mheshimiwa Dkt. Makame Ali Ussi

13. WIZARA YA UJENZI, MAWASILIANO NA USAFIRISHAJI

i. Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji – Mheshimiwa Dkt. Sira Ubwa Mamboya

ii. Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji – Mheshimiwa Mohamed Ahmada Salum

14. WIZARA YA VIJANA, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

i. Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo - Mheshimiwa Balozi Ali Abeid Karume

ii. Naibu Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo - Mheshimiwa Lulu Msham Abdulla



Aidha, Mheshimiwa Said Soud Said na Mheshimiwa Juma Ali Khatib wanaendelea kuwa Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi na Mawaziri Wasiokuwa na Wizara Maalum.


WAKATI huo huo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi na kuwabadilisha nafasi baadhi ya viongozi katikaTaasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kama ifuatavyo:-

1. UTEUZI WA WAKUU WA WILAYA

i. Bwana Issa Juma Ali ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkoani, Pemba.

ii. Bwana Rajab Ali Rajab ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B, Unguja.

2. UTEUZI WA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA NA WILAYA

i. Bwana Bakari Ali Bakari ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa Kaskazini, Pemba.

ii. Bibi Fatma Mohamed Juma ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa Kusini, Unguja.

iii. Bwana Juma Abdulla Hamad ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Mjini.

iv. Bwana Hamza Mahmoud Ibrahim ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Magharibi B.

v. Bwana Makame Machano Haji ameteuliwa kuwa Katibu Tawalawa Kaskazini B.


3. UTEUZI WA OFISA MDHAMINI WA WIZARA YA AFYA - PEMBA

i. Bibi Shadya Shaaban Seif ameteuliwa kuwa Ofisa Mdhaminiwa Wizara ya Afya – Pemba.

4. UTEUZI WA MWENYEKITI NA MKURUGENZI MKUU WA WAKALA  WA MAENDELEO YA VIWANDA VIDOGO VIDOGO NA VYA KATI

i. Bwana Mussa Ame Silima ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maendeleo ya Viwanda Vidogo Vidogo na vya Kati.

ii. Bwana Abdulhamid Idrisa Haji ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Viwanda Vidogo Vidogo na vya Kati.

5. UTEUZI WA MKURUGENZI WA TAASISI YA KARUME YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA

Dr. Mustafa Ali Garu ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia.

6. UTEUZI WA MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA MAJI (ZAWA)

Bwana Mussa Ramadhani Haji ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Kuu wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA).

7. UTEUZI WA MWENYEKITI WA BODI NA WATENDAJI WA WAKALA WA MATUKIO YA KIJAMII

i. Bwana Haji Machano ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii.

ii. Dkt. Hussein Khamis Shaaban ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii.

iii. Bwana Idrisa Shaaban Zaharan ameteuliwa kuwa Naibu Mkurugenzi Mtendaji anaehusika na Usajili wa Mzanzibari Mkaazi na Wageni Wakaazi katika Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii.

iv. Bwana Shaaban Ramadhan Abdulla ameteuliwa kuwa Naibu Mkurugenzi Mtendaji anaeshughulikia Usajili wa Vizazi, Vifo, Ndoa na Talaka.

8. UTEUZI WA MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI YA PBZ

Bibi Kidawa Hamid Saleh ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya PBZ.

Uteuzi huo unaanza tarehe 1Machi, 2018.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.