Habari za Punde

Rais Dk Shein amtumia salamu za Pongezi Kiongozi wa KuwaitSTATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
  Zanzibar                                                            24.02.2018
---
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein amemtumia salamu za pongezi Kiongozi wa Taifa la Kuwait, Sheikh Sabah Ahmad Al-Sabah kwa kuadhimisha miaka 57 ya siku ya uhuru wa Taifa hilo.

Salamu hizo zilieleza kuwa wananchi wa Zanzibar wanaungana na ndugu zao wa Kuwait katika kusherehekea siku hii adhimu kwa Taifa hilo.

Aidha, katika salamu hizo, Dk. Shein alimuhakikishia Sheikh Sabah Ahmad Al-Sabah kuwa Zanzibar itaendeleza uhusiano na ushirikiano uliopo kati yake na Kuwait.

Dk. Shein alimtakia kiongozi huyo na familia yake pamoja na wananchi wote wa Kuwait afya njema na sherehe njema katika kuadhimisha siku hiyo ya Taifa sambamba na kumtakia mafanikio zaidi katika kuendelea kuipatia maendeleo zaidi ya kiuchumi nchi hiyo kwa madhumuni ya kulinufaisha Taifa hilo na wananchi wake.

Kuwait inasherehekea siku yake ya Taifa kila ifikapo Februari 25 ya kila mwaka ambapo nchi hiyo ilipata uhuru wake kutoka kwa Wakoloni wa Kiengereza mnamo mwaka 1961 chini ya Jemedari wa Taifa hilo Marehemu Sheikh Abdallah Al-Salem Al-Sabah aliyefariki dunia mnamo mwaka 1965.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.