Habari za Punde

SEMINA KUHUSU MAPENDEKEZO YA KUTUNGWA SHERIA YA KULINDA TAARIFA BINAFSI KWA WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI YAFANYIKA ZANZIBAR.

Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Mgeni Hassan Juma akitoa hotuba ya Ufungaji wa Semina  ya  Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuhusu  Mapendekezo ya kutungwa kwa Sheria ya kulinda taarifa binafsi iliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean View  Kilimani mjini Unguja. 
Naibu Waziri  Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Tanzania Mhe, Atashasta Nditiye  akitoa hotuba katika Semina ya  Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuhusu  Mapendekezo ya kutungwa kwa Sheria ya kulinda taarifa binafsi iliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean View  Kilimani mjini Unguja
 Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waliohudhuria katika Semina kuhusu mapendekezo ya kutungwa kwa Sheria ya kulinda taarifa binafsi ilioandaliwa na Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Tanzania iliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean View  Kilimani mjini Unguja.
 Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waliohudhuria katika Semina kuhusu mapendekezo ya kutungwa kwa Sheria ya kulinda taarifa binafsi ilioandaliwa na Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Tanzania iliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean View  Kilimani mjini Unguja.
 Mwanasheria Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliani Tanzania Eunice Masigati akiwasilisha mada kuhusu Mapendekezo ya kutungwa kwa Sheria ya kulinda taarifa binafsi katika semina ya Wajumbe wa Baraa la Wawakilishi  iliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean View  Kilimani mjini Unguja. 
 Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe,Zuberi Ali Maulid katikati akizungumza katika semina ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuhusu  Mapendekezo ya kutungwa kwa Sheria ya kulinda taarifa binafsi iliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean View  Kilimani mjini Unguja. 
 Muakilishi wa Jimbo la Paje  Jaku Hashim Ayoub akitoa mchango wake pamoja na kuuliza maswali katika Semina  kuhusu mapendekezo ya kutungwa kwa Sheria ya kulinda taarifa binafsi ilioandaliwa na Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Tanzania iliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean View  Kilimani mjini Unguja.
 Muakilishi wa Jimbo la Kwamtipura Hamza Hassan Juma akitoa mchango wake pamoja na kuuliza maswali katika Semina  kuhusu mapendekezo ya kutungwa kwa Sheria ya kulinda taarifa binafsi ilioandaliwa na Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Tanzania iliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean View  Kilimani mjini Unguja. 
 Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Balozi Ali Karume akitolea ufafanuzi baadhi ya maswali yalioulizwa katika Semina ya  Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuhusu  Mapendekezo ya kutungwa kwa Sheria ya kulinda taarifa binafsi iliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean View  Kilimani mjini Unguja. 

Na Kijakazi Abdalla,  Maelezo Zanzibar 10/02/2018
NAIBU waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye amesema kumeibuka uhalifu unaowezeshwa na upatikanaji rahisi wa taarifa binafsi ambazo huhatarisha maisha ya watu na mali.
Hayo aliyasema katika mkutano wa kuwasilisha mapendekezo ya kutunga sheria ya kulinda taarifa binafsi kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar huko Zanzibar Ocean View Kilimani.
Amesema kuwa kutokana na maendeleo ya Tehama kila siku kiasi kikubwa cha taarifa binafsi kinakusanywa na kuhifadhiwa ambapo pamoja na matumizi mazuri ya taarifa hizo.
Aidha alisema kuwa ulinzi unahitajika ili kujenga misingi mizuri ya matumizi ya taarifa binafsi katika jamii ambapo kunapelekea uhitaji wa sheria ambayo inahitaji muongozo wa ukusanyaji ,utunzaji na usambaji wa taarifa binafsi.
Alisema kuwa teknojia imekuwa na inahitaji kuwa na sheria ambayo inayopendekeza itatumia pande zote mbili ya jamuhuri ya muungano na machakato wake ulianza wa kutunga sheria na vikao mbalimbali vimekuwa vikifanyika tangu mwaka 2009.
Hata hivyo Mhandisi Nditiye alisema kuwa misingi mikubwa ya kutunga sheria ni utekelezaji wa Ibara ya 16 ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Ibara ya 15 ya Katiba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Aidha alisema kuwa sheria iliyopendekezwa ni ya usalama wa mtandao kutokana na ukikwaju wa teknolojia ambayo imeridhiria miongozo inyoelekeza nchi kuwa na sheria hiyo.
Nae Mwanasheria wa sekta ya Mawasiliano Eunice Masigati amesema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoathirika na uhalifu wa mitandao ikiwemo uhalifu unaotokana na matumizi mabaya ya taarifa binafsi.
Hivyo alisema kwamba usimamizi wa kisheria wa masuala yanayohusu udhibiti wa matumizi na ufikiaji wa taarifa zilizopo kwenye mifumo ya kompyuta na mitandao kwa ujumla.
Aidha alisema kuwa kulinda taarifa binafsi itahusu udhibiti wa namna ambavyo taarifa za mtu,kampuni au serikali zinavyoweza kutumika kwa kuwa na umuhimu wa kutunga sheria ambayo itapendekezwa kulinda taarifa binafsi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.