Habari za Punde

Sumeit University waanzisha Advance School kidatu cha Tano kuanzia mwaka huu

Chuo kikuu cha Sumait kinawatangazia wanafunzi wote waliomaliza masomo yao ya kidatu cha nne mwaka 2017 kwamba wanaanzisha advance school  yaani kidatu cha tano mwaka huu.

Masomo yataanza rasmi mwezi wa nne hapo hapo Chukwani Campus. 

Sifa za kujiunga ni division 1, 2 na 3 science na arts subject. 

Kwa maelezo zaidi fika Sumait University iliyopo Chukwani.  Pia tunakaribisha maombi ya kazi kwa walimu wenye uwezo wa kufundisha advance level kwa masomo yote.

Sifa za muombaji 

1. Angalau awe na degree moja na kuendelea ya masomo husika,  GPA not less than  3.5. Division one ya form 4 na 6.

2.      Uzoefu usipungue miaka mitano.

Pia  chuo kinakaribisha maombi ya kufundisha Cheti na Diploma kwa course zifuatazo.

1. Accountancy, 
2. Public administration,
3. Archive and Record management,
4. Community development, 
5. Procurement and supply,
6. Computing information and communication technology. 


Shukran

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.