Habari za Punde

UAE Kujenga Nyumba 55 Kwa Wananchi Waliopata Maafa Unguja na Pemba.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohammed  Aboud Mohammed kulia akizungumza na Ujumbe wa  Mwezi Mwekundu wa  Emarates kuhusiana na utiliaji saini Ujenzi wa Nyumba za msaada kwa waathirika wa mafuriko Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohammed  Aboud Mohammed aliesimama kulia akiwa pamoja na Msaidizi Balozi wa Emarates Muhammed Ibrahim Al-Bahri wakishuhudia utiaji saini  Ujenzi wa Nyumba za msaada kwa waathirika wa mafuriko Zanzibar.
Mkurugenzi wa Kamisheni ya Maafa zanzibar Shaaban Seif Mohammed akibadilishana hati ya saini na Mkurugenzi wa Maafa wa Emarates Said Mohammed Al-humaini kuhusiana na  Ujenzi wa Nyumba za msaada kwa waathirika wa mafuriko Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohammed  Aboud Mohammed akiwa katika picha ya pamoja na  Ujumbe wa  Mwezi Mwekundu wa  Emarates baada ya  kutiliana  saini Ujenzi wa Nyumba za msaada kwa waathirika wa mafuriko Zanzibar.
Picha na Yussuf Simai - Maelezo Zanzibar.
Na Miza Kona-Maelezo Zanzibar.
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetiliana saini ya makubaliano na Serikali ya Nchi za Falme za Kiarabu (UAE), kuhusiana na ujenzi wa nyumba kwa ajili ya wananchi ambao makaazi yao yaliharibika kutokana na mvua za masika.
Hafla hiyo  ya utilianaji wa saini hiyo umefanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Vuga Zanzibar. kati ya Mamlaka ya Mwezi Mwekundu ya UAEitakayoshughulikia ujenzi huo na Kamisheni ya Maafa ya Zanzibar.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohammed Aboud Mohammed, amesema msaada wa ujenzi huo ni matunda ya ziara iliyofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein katika Nchi za Umoja wa Nchi za  Falme za Kiarabu mwezi ulipita.
Katika ziara hiyo, Mfalme wa UAE aliahidi kuisaidia Zanzibar katika sekta mbalimbali za maendeleo na huduma za kijamii. 
“Tunaishukuru serikali ya UAE kwa msaada huu mkubwa ambao utazidikuimarisha uhusiano na udugu uliopo baina ya nchi zetu,”alisema Aboud.
Nae Mkurugunzi wa kamisheni ya kukabiliana na Maafa Shaaban Seif Mohammed,amesema msaada huo utasaidia kuondoa usumbufu wanaopata wananchi katika kipindi cha mvua hasa yanapotokea mafuriko.
Wananchi wanaoishi maeneo ya Ziwa Maboga, Mwanakwerekwe na mengine yanayotuwama maji ndio watakaohamishiwa kwenye nyumba hizo ili wakae katika makaazi salama,” alisema.
Aidha nyumba zilizojengwa katika maeneo yenye kupita au kukaa maji tutazivunja ili kukomesha maafa na usumbufu,”alieleza Mkurugenzi huyo.
Mkurugenzi huyo amewataka wananchi kuchukua tahadhari za mapema kwa kuondoka maeneo yanayokaa maji ili kuepuka na hasara na matatizo wakati wa kipindi cha mvua.
Nae mwakilishi kutoka ubalozi wa UAE Mohammed Ibrahim Al-Bahr, amesema serikali ya nchi yake itaendelea kuisaidia Zanzibar kwa kuimarisha huduma za kijamii ikiwemo hospitali na uchimbaji wa visima kwa lengo la kuwasaidia wananchi wake pamoja na kutemaendelea.
Ameishukuru Serikali ya Zanzibar kwa kuwapatia ardhi itakayotumikakujenga nyumba za makaazi ya kudumu kwa ajili ya wananchi waliokumbwa na maafa ili waishi kwa furaha na utulivu.
Mradihuoutahusishanyumba 55 ambapo 30 zitajengwaFukuchaniMkoawaKaskaziniUnguja, nanyengine 25 zitajengwaTumbeMkoawaKaskaziniPemba. 
                                         MWISHO.
                 IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

1 comment:

  1. Mnaleta warabu watakupindueni.
    Baniani mbaya kiatu chake dawa

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.