Habari za Punde

Wachezaji wa Zanzibar Heroes wakabidhiwa viwanja vya Plan Tunguu

Mlinda mlango wa Zanzibar Heroes, Ahmed Salula akikabidhiwa kiwanja hati ya kiwanja chake huko Tunguu katika utekelezaji wa ahadi ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein aliyoitoa Disemba 23, 2017 na Waziri wa ardhi, maji, nishati na mazingira Salama Aboud Talib.

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Wachezaji na Viongozi 33 wa Timu ya Taifa ya Soka ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) wamekabidhiwa hati zao za viwanja walivyoahidiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein aliyoitoa Disemba 23, 2017.
Wakikabidhiwa Viwanja hivyo eneo la Tunguu Plan na Waziri wa ardhi, maji, nishati na mazingira Salama Aboud Talib amewataka kuvienzi na kuvitunza kama walivyoagizwa na Dkt Shein kuwa wasiviuze bali wavitumie katika kujenga maisha yao.
Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inathamini Michezo ndio maana ikawazawadia viwanja pamoja na zawadi mbali mbali.
Nae waziri wa habari utalii utamaduni na michezo Rashid Ali Juma amesema leo ni siku ya historia kwa mashujaa hao baada ya kukabidhiwa rasmi viwanja vyao walivyoahidiwa na rais wa zanzibar na kuwahimiza kuendelea kujituma kwani michezo ni ajira.
Kwa upande wake kocha mkuu wa timu hiyo Hemed Suleiman (Morocco) amemshukuru Dkt Shein kwa ahadi yake kutimizwa leo huku wakiwa nafura kubwa sana kwa tukio hilo.
Wachezaji wa timu hiyo wamefurahishwa baada ya Rais wa Zanzibar kutimiza ahadi yake ya kuwapatia na kumpongeza kwa juhudi zake za kupenda na kuthamini michezo.

Zanzibar Heroes ilifanikiwa kushika nafasi ya pili katika Mashindano ya Cecafa Senior Chalenj Cup Mwaka jana baada ya kufungwa kwa penalty 3-2 na wenyeji Kenya baada ya kutoka sare ya 2-2 ndani ya dakika 120.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.