MAKAMU
Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa shirika la bandari Zanzibar, Khamis Silima
Ali mwenye kalamu, akionyeshwa ramani ya eneo la bandari katika mnara wa kuongozea
Meli za kimataifa ulioko Kigomasha Makangale Wilaya ya Micheweni, wakati
wajumbe wa bodi hiyo walipofanya ziara ya kutembelea maeneo yaliyochini ya
shirika hilo.(PICHA NO:ABDI SULEIMAN,
PEMBA)
WAJUMBE
wa bodi ya wakurugenzi wa shirika la bandari Zanzibar, wakionyeshwa mipaka ya
eneo la mnara wa kuongozea meli za kimataifa ulioko Kigomasha Makangale Wilaya
ya Micheweni, kutoka kwa mkuu wa kituo hicho Yahaya Hassan, wakati wajumbe hao
walipofanya ziara ya kukagua maeneo yaliyochini ya shirika hilo upande wa Pemba.(PICHA NO:ABDI SULEIMAN, PEMBA)
WAJUMBE
wa bodi ya wakurugenzi wa shirika la bandari Zanzibar, wakiongozwa na Makamu
mwenyekiti wa bodi hiyo Khamis Salim Ali, wakikagua mipaka ya eneo la Mnara wa
Kigomasha Makangale, mnara huo ambao hutumika kuongoza meli za kimataifa.(PICHA NO:ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MKURUGENZI
Mkuu wa Shirika la bandari la Zanzibar Abdalla Juma Abdalla, akitoa maelekezo
juu ya bandari ya Wete kwa wajumbe wa bodi ya wakurugenzi ya shirika la
bandari, wakati wajumbe hao walipofanya ziara ya kutembelea meneo ya shirika
hilo.(PICHA NO:ABDI SULEIMAN, PEMBA)
INJINIA
Mkuu wa shirika la bandari la Zanzibar Mbarouk Hamad Mbarouk, akitoa maelezo ya
kitaalamu juu ya bandari yaw ate, kwa wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa shirika
la bandari Zanzibar, wakati walipofanya ziara ya kutembelea maeneo mbali mbali
yaliyochini ya bandari tawi la Pemba.(PICHA
NO:ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MKURUGENZI
wa shirika la Bandari tawi la Pemba Hamad Salim Hamad, akimuelezea jambo Makamu
Mwenyekiti wa bodi ya shirika la Bandari Zanzibar, wakati alipotembelea bandari
ya wete katika ziara yao ya kukagua maeneo ya shirika hilo Pemba.(PICHA NO:ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MMOJA
ya nyumba za TRA ambazo zimeshachakaa katika bandari ya Wete, ambazo bodi ya
wakurugenzi wa shirika la bandari Zanzibar, wameagiza nyumba hizo kurudishwa
kwenye shikila la bandari.(PICHA NO:ABDI
SULEIMAN, PEMBA)
WATENDAJI
wa Shirika la bandari Tawi la Pemba, wakimuonyesha Makamu Mwenyekiti wa bodi ya
wakurugenzi wa shirika la Bandari Zanzibar, mipaka ya eneo la bandari ya Wete
wakati wajumbe hao walipofanya ziara ya kukagua eneo la bandari hiyo.(PICHA NO:ABDI SULEIMAN, PEMBA)
WATENDAJI
wa Shirika la bandari Tawi la Pemba, wakimuonyesha Makamu Mwenyekiti wa bodi ya
wakurugenzi wa shirika la Bandari Zanzibar, mipaka ya eneo la bandari ya Wete
wakati wajumbe hao walipofanya ziara ya kukagua eneo la bandari hiyo.(PICHA NO:ABDI SULEIMAN, PEMBA)
No comments:
Post a Comment