Habari za Punde

Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Aendelea na Ziara Yake Kutembelea Vyombo vya Habari Zanzibar.

Afisa wa Shirika la Magazeri ya Serikali Zanzibar Leo Chumba cha Habari Juma Mohammed akitowa maelezo kwa Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi ya CCM Zanzibar Bi. Catherine Peter, wakati wa muendelezo wa ziara yake kutembelea vyombo vya habari mbalimbali Zanzibar  
Katibu Msaidi wa Idara ya Idara ya Utawala CCM Zanzibar Daud Ismail, akizungu wakati wa ziara yao hiyo wakitembelea Shirika la Magazeti la Zanzibar Leo, maisara Zanzibar.kushoto Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Catherine Peter na wa mwisho Mharariri Mtendaji wa Gazeti la Zanzibar leo Yussuf Khamis.  
Mhariri Mtendaji wa Shirika la Magazeti ya Serikali Zanzibar leo Yussuf Khamis akizungumza wakati wa ziara ya Ujumbe wa Katibu wa Idara ya Itikadin na Uenezi ya CCM Zanzibar walipofika kutembelea Gazeti hilo kujionea utendaji kazi wao katika majengo ya Ofisi zao maisara Zanzibar.
Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Catherine Peter akizungumza na wafanyakazi na Wakuu wa Gazeti la Zanzibar leo wakati wa ziara yake kutembelea vyombo mbalimbali vya habari zanzibar, akiwa katika muendelezo wake katika kutembelea vyombo mbalimbali baada ya kuchaguliwa kwake kushika nafasi hiyo mwezi uliopita.
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.