Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Bill and Melinda Gates Foundation Bw. Rodger Voorhies kwenye Makazi ya Makamu wa Rais, Kilimani mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 23 Machi, 2018 amekutana na
kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Bill & Melinda
Gates Foundation Bw. Rodger Voorhies kwenye makazi ya
Makamu wa Rais, Kilimani
mjini Dodoma.
Makamu wa Rais amesema amezungumza mambo
mengi na Bw. Rodger hasa kwenye masuala ya afya, uwezeshaji wanawake kiuchumi,
kuwatoa kwenye kilimo cha sasa na kuwaingiza kwenye kilimo biashara lakini pia
kuongeza thamani ya mazao na mambo ya masoko.
Makamu wa Rais alisema wamezungumza namna ya
kuwarasimisha wanawake wa vijijini na wanawake wakulima ikiwa pamoja na
uwezekano wa wanawake vijijini kuweza kupata mikopo.
Aidha Makamu wa Rais alizungumzia suala zima
la upatikanaji wa maji safi na salama haswa kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam
ambapo mara kwa mara kumekuwa na milipuko ya magojwa ya kipindu pindu.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya Bill & Melinda Gates Foundation Bw. Rodger Voorhies alisema
wamekuja kwa Makamu wa Rais kuzungumza juu ya shughuli zinazofanywa na taasisi
hiyo hapa nchini haswa katika masuala ya Kilimo na Afya na Mkakati Mpya wa
Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi.
Aidha wameipongeza Serikali ya Tanzania kwa
hatua kubwa ambayo wamepiga katika kuwajumuisha wanawake katika masuala
yanayohusu Fedha.
Mwisho, Mkurugenzi huyo ameahidi ushirikiano
mkubwa kwa Serikali ya Tanzania katika kutekelezaji wa miradi ya taasisi yao.
No comments:
Post a Comment