Habari za Punde

MASAUNI AZINDUA VITUO MWENDO SITA VYA POLISI,AWAASA WANANCHI KUJIKITA KWENYE SHUGHULI ZA MAENDELEO

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akisikiliza maelezo ya Kituo Mwendo cha polisi kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Jumanne Muliro (katikati), baada ya kuzindua moja ya vituo hivyo ambavyo idadi yake ni sita, lengo ikiwa vitumike katika maeneo ya mkoa huo kudhibiti uhalifu. Kulia ni Kamanda wa Kanda Maalumu ya Polisi Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa. Tukio hilo limefanyika leo, jijini Dar es Salaam. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Vituo Mwendo sita vya polisi ambavyo vimegawiwa kwa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni ili kuweza kuzuia na kupambana na uhalifu huku akiwaasa wananchi kujikita kwenye shughuli za maendeleo. Tukio hilo limefanyika leo, jijini Dar es Salaam. 
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi,Nsato Marijani akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Vituo Mwendo sita vya polisi ambavyo vimegawiwa kwa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni ili kuweza kuzuia na kupambana na uhalifu . Tukio hilo limefanyika leo, jijini Dar es Salaam
Kamanda wa Kanda Maalumu ya Polisi Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Vituo Mwendo sita vya polisi ambavyo vimegawiwa kwa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni ili kuweza kuzuia na kupambana na uhalifu . Tukio hilo limefanyika leo, jijini Dar es Salaam
 Askari wa Kikundi cha Ulinzi Shirikishi kutoka Mkoa wa Polisi Kinondoni, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani), wakati wa Uzinduzi wa Vituo Mwendo sita vya polisi ambavyo vimegawiwa kwa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni ili kuweza kuzuia na kupambana na uhalifu. Tukio hilo limefanyika leo, jijini Dar es Salaam

Moja ya Vituo Mwendo vya Polisi vilivyozinduliwa leo na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani), ambavyo vitatumika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kipolisi Kinondoni katika kuzuia na kupambana na uhalifu. Tukio hilo limefanyika leo, jijini Dar es Salaam Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI -WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.