Habari za Punde

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba akerwa na matokeo mabaya kwa skuli za Pemba

Na Salmin Juma, Pemba

Mkuu wa mkoa wa Kusini Pemba Mh Hemed Suleiman Abdalla ameonekana kutofurahia kabisa na jinsi ya matokeo ya wanafunzi wa mwaka jana kwa skuli za Pemba kutofanya vizuri kidato cha nne na vyenginevyo hali iliyopelekea kuonekana kuwa kiwango cha elimu nchini kimeshuka.

Akizungumza na walimu wakuu wa skuli mbalimbali pamoja na wenyeviti wa kamati za skuli na wadau wengine wa setka ya elimu katika mkoa wake jana huko katika ukumbi wa skuli ya Fidel Castro wilaya ya chakechake  Mh Mkuu wa mkoa amesema kuna haja ya kuziona shahada zote za walimu ili ajiridhishe kutokana na kuwa na wasiwasi na viwango vyao vya elimu.

"Wapo walimu wenye shahada na stashahada za vyuo vyenye majina makubwa lakini bado skuli watoto wanaambulia zero hivyo elimu yao bado haiwasaidii watoto kwa kutokuwa na maarifa na miongozo na mikakati mizuri katika ufundishaji lakini pia nataka kuziona shahada zao wote"

Aidha Mh Hemed amesema, jambo la kusitikisha ni kuwa , masomo ya dini ndio masomo wanayofaulu vizuri wanafunzi kila mwaka lakini mwaka uliyopita hata hayo  wameshindwa kufaulu.

"Matokea ya aslimia 73 kwenye 100  katika kufanya vibaya haya huitwa matukio hasi ikibaki chanya 27 , matukio haya ni mabaya kwa sual la Ellimu Wilaya ya Chake Chake"

Mh Hemed amesema katika skuli za Sekondari Wilaya ya Chake ni skuli tatu pekee zilizofanya vizuri ikiwemo Fidel Castro, Madungu Sekondari na Skuli ya Connecting ambayo ni ya binafsi.

Katika hatua nyengine Mh Mkuu wa Mkoa amesema, ni lazima kufanyike jitihada za makusudi ili kuona hali ya upasishaji wanafunzi inakua katika kiwango cha juu na yeye kama mkuu wa mkoa atalisimamia hilo ili kulifanikisha

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.