Habari za Punde

Naibu Waziri Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Azungumza na Walimu wa Sayansi Kutoka Nchini Nigeria.

Mkurugenzi wa Elimu Sokondari Zanzibar Bi. Asya akizungumza wakati wa mkutano wa kuwatambulishwa Walimu wa masomo ya Hesabati na Fizikia kutoka Nchini Nigeria waliofika Zanzibar kufundisha Wanafunzi wa Skuli za Sekondari za Unguja na Pemba, walimu wahi 16 wamewasili Zanzibar na jumla yao 39 wataungana na Walimu ya Zanzibar kutowa Elimu hiyo kwa Wanafunzi wa Skuli za Sokondari Zanzibar, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Mazizini Zanzibar. baada ya kuwasili jana.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Mmanga Mjengo Mjawiri akizngumza na Walimu wa masomo ya Hesabati na Fizikia walipofika katika Ofisi za Wizara ya Elimu mazizini Zanzibar kujitambulia baada ya kuwasili kuaza kazi hiyo Zanzibar kufundisha Wanafunzi wa Skuli za Sekondari za Unguja na Pemba.
Mkurugenzi Programu kutoka Nigeria Kiongozi wa Msafara huo Mr. J.A.Oduniyi akizungumza wakati wa mkutano huo wa kuwatambulisha walimu hao kwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Mmanga Mjengo Mjawiri, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Wizara mazizini Zanzibar. 
Mkuu wa Msafara wa Walimu 16 kati ya 39 wanaotarajiwa kuwasili Zanzibar kwa ajili ya kufundisha Skuli za Sekondari za Unguja na Pemba Mr. J.A.Oduniyi akizungumza na Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe. Mmanga Mjengo Mjawiri baada ya hafla ya kutambulishwa Walimu hao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.