Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein Amefanya Uteuzi wa Makatibu Wakuu na Manaibu na Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar.


Kufuatia mabadiliko ya Wizara za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliofanyika hivi karibuni, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi na kuwabadilsha wadhifa baadhi ya watendaji wakuu katika taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kama ifuatavyo:

1. OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS
   Bwana Shaaban Seif Mohamed ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu katika Ofisi ya Makamu         wa Pili wa Rais.

2. WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI
Dkt. Idrissa Muslim Hija ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali

3. WIZARA YA HABARI, UTALII NA MAMBO YA KALE

i. Bibi Khadija Bakari Juma ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu katika Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale.

ii. Dkt. Saleh Yussuf Mnemo ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale anayeshughulikia masuala ya habari.

iii. Dkt. Amina Ameir Issa ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika  Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale anaeshughulikia masuala ya Utalii na Mambo ya Kale.

4. WIZARA YA VIJANA, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

i. Bwana Omar Hassan Omar ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu katika Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

ii. Bwana Amour Hamil Bakari ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo

5. WIZARA YA KILIMO, MALIASILI, MIFUGO NA UVUVI

i. Bibi Maryam Juma Abdalla Saadalla ameteuliwa Katibu Mkuu katika  Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi

ii. Bwana Ahmad Kassim Haji ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi anaeshughulikia masuala ya Kilimo na Maliasili

6. WIZARA YA BIASHARA NA VIWANDA

i. Bwana Juma Ali Juma ameteuliwa Katibu Mkuu katika  Wizara ya Biashara na Viwanda

ii. Bwana Ali Khamis Juma ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika   Wizara ya Biashara na Viwanda.

7. WIZARA YA KAZI, UWEZESHAJI, WAZEE, WANAWAKE NA WATOTO

i. Bibi Fatma Gharib Bilal ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu katika  Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto

ii. Bibi Maua Makame Rajab ameteuliwa kuwa Naibu katibu Mkuu katika  Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wanawake na Watoto anaeshughulikia masuala ya Kazi na Uwezeshaji.

iii. Bibi Mwanajuma Majid Abdulla ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika  Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto anaeshughulikia masuala ya Wazee, Wanawake na Watoto.


8. WIZARA YA ARDHI, NYUMBA, MAJI NA NISHATI

i. Bwana Ali Khalil Mirza ameteuliwa Katibu Mkuu katika  Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati.

ii. Bwana Tahir M. K. Abdulla ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika   Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati


9. BODI YA MAPATO YA ZANZIBAR

Bwana Joseph Abdalla Meza ameteuliwa kuwa Kamishna wa Bodi ya Mapato ya Zanzibar (ZRB).


10. BENKI YA WATU WA ZANZIBAR

Bibi Khadija Shamte Mzee ameteuliwa kuwa Naibu Mkurugenzi Mtendajii wa Benki ya Watu wa Zanzibar.
Uteuzi huo unaanza tarehe 12 Machi 2018.
Makatibu na Naibu Makatibu Wakuu waliotajwa pamoja na Kamishna wa Bodi ya Mapato wanatakiwa waripoti Ikulu siku ya Jumanne  tarehe 13 Machi 2018, saa 2:30 asubuhi tayari kwa kuapishwa.

(Dkt. Abdulhamid Y. Mzee)
Katibu wa Baraza la Mapinduzi na
Katibu Mkuu Kiongozi
Zanzibar.
TAREHE 10 MACHI, 2018

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.