Habari za Punde

Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa shirika la Bandari Zanzibar wakiendelea na ziara yao kisiwani Pemba

 WAJUMBE wa Bodi ya Wakurugenzi wa shirika la Bandari Zanzibar, wakiwasili katika mnara wa kuongozea meli Matumbilini, wakati wa ziara yao Kisiwani Pemba ya kuangalia shuhuli mbali mbali zilizochini ya shirika la Bandari Tawi la Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA.)
 WAJUMBE wa Bodi ya Wakurugenzi wa shirika la Bandari Zanzibar, wakiteremka katika faiba iliyowasafirisha kutoka bandarini Mkoani hadi katika mnara wa matumbilini, katika ziara yao ya kuangalia shuhuli mbali mbali zilizochini ya shirika hilo Tawi la Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA.)

  MNARA wa Matumbilini ni moja ya minara mikubwa katika Kisiwa cha Pemba, inayoongoza meli mbali mbali zinazopita katika eneo hilo, mnara huo umepewa Namba ya Kimataifa K0451 ukiwa na urefu Mita 29 kutoka usawa wa aridhini kwenda juu.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA.)
 Kepteni Makame Hassan Ameir kutoka Shirika la Bandari la Zanzibar, akitoa maelekezo juu ya mnara wa matumbilini kwa wajumbe wa bodi ya shirika la bandari, wakati wajumbe hao walipotembelea maeneo yaliyochini ya shirika hilo Tawi la Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA.)
 MLINZI wa Mnara wa kuongozea meli Matumbilini ulioko Kisiwani Pemba, Makame Ame Khatib akitoa maelekezo jinsi mnara huo unavyotoa huduma zake kwa meli zinazopita baharini, pamoja na miwako yake wakati walipofika katika mnara huo.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA.)

MUONEKANO wa Nje wa Mnara wa kuongozea meli Matumbilini Kisiwani Pemba, wakati wajumbe wa bodi ya shirika la bandari walipotembelea mnara huo.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA.)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.