Habari za Punde

Waziri Mwakyembe amtembelea na kumjuulia hali Rais wa zamani wa ZFA, Ali Ferej Tamim

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe akisalimiana na mtoto wa mzee Ali Ferej Tamim, Bi Rasmiya Ferej
Mzee Ali Ferej Tamim mbae kwa sasa ni mgonjwa akizungumza na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na michezo wa SMT Dkt Harrison Mwakyembe wakati alipoomtembelea nyumbani kwake huku akishuhudia ni Waziri wa Habari wa SMZ Mahmoud Thabit Kombo pamja na mtoto wa Mzee Ali Ferej Tamim, Bi Rasmiya Ferej

Na Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Tanzania Dkt Harrison Mwakyembe amemjulia hali Rais wa zamani wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) Ali Ferej Tamim nyumbani kwake Shangani Mjini Unguja ambae anasumbuliwa na Uti wa Mgongo.

Mwakyembe ambaye ameongozana na Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya kale Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo, Katibu wa Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sana na Michezo Omar Hassan (King) na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Simai Mohammed Said.

Mwakyembe amesema ameona haya ya kumtembelea mwana michezo huyo kutokana na kazi kubwa aloifanya katika taifa la Tanzania.

Nae Katibu wa Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sana na Michezo Omar Hassan (King) amesema kutokana na kuongoza vyema ZFA pamoja na kuitangaza Zanzibar kimataifa wameona haja ya kumtembelea.

Kwa upande wake Rais wa zamani wa ZFA Ali Ferej Tamim amewashukuru na kuwapongeza viongozi hao kwenda kumjulia hali huku akisema kwasasa amepata afadhali na kuendelea kufata ushauri wa Daktari.

Mapema leo Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Tanzania Dkt Harrison Mwakyembe amekutana na Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya kale Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo pamoja na Waziri wa Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sana na Michezo Ali Karume kwa lengo la kujuwana na kupanga mikakati yao ikiwemo masuala ya michezo yanayogusa pande zote mbili za Muungano wa Tanzania.

1 comment:

  1. Mwandishi wa habari hii huna maana pesa mbili, hivi huyu Mwakyembe ni Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo wa Tanzania????!!! Wazanzibsri bado tunayo kazi kubwa mpaka kujikomboa.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.