Habari za Punde

Samia ataka jamii isiwapuuze watoto yatima

 Baadhi ya Watoto mayatima waliohudhuria katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto yatima yaliofanyika katika Viwanja vya Bakhresa Fumba Wilaya ya Magharibi B Unguja.

 Baadhi ya Watoto mayatima waliohudhuria katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto yatima yaliofanyika katika Viwanja vya Bakhresa Fumba Wilaya ya Magharibi B Unguja.

 Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wanawake Wazee na Watoto Maudline Cyrus Castico akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kiislamu ya Muzdalifa Farouk Hamad Khamis mara Baada ya kuwasili katika  maadhimisho ya Siku ya Mtoto yatima yaliofanyika katika Viwanja vya Bakhresa Fumba Wilaya ya Magharibi B Unguja.

 Watoto mayatima kutoka Skuli ya Alfarouk Aktas Muslim wakisoma Kasda maalum yenye maudhui ya kumlinda mtoto yatima katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto yatima yaliofanyika katika Viwanja vya Bakhresa Fumba Wilaya ya Magharibi B Unguja.
  Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kiislamu ya Muzdalifa Farouk Hamad  Khamis akizungumza machache kuhusu mtoto yatima katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto yatima yaliofanyika katika Viwanja vya Bakhresa Fumba Wilaya ya Magharibi B Unguja.

 Watoto mayatima kutoka Skuli ya Alfarouk Aktas Muslim wakionesha mchezo wa sarakasi  katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto yatima yaliofanyika katika Viwanja vya Bakhresa Fumba Wilaya ya Magharibi B Unguja. 

 Mwakilishi wa Balozi wa Uturuki Nchini Tanzania Oguz Hamza Yilmaz akitoa maelezo kuhusu mtoto yatima  katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto yatima yaliofanyika katika Viwanja vya Bakhresa Fumba Wilaya ya Magharibi B Unguja.  

 Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Swaleh Omar Kabi akitoa hotuba yamakaribisho kwa mgeni rasmi  katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto yatima yaliofanyika katika Viwanja vya Bakhresa Fumba Wilaya ya Magharibi B Unguja.   

 Mgeni rasmi Waziri wa  Kazi Uwezeshaji Wanawake Wazee na Watoto Maudline Cyrus  Castico akitoa Hotuba  katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto yatima yaliofanyika katika Viwanja vya Bakhresa Fumba Wilaya ya Magharibi B Unguja.    

Mgeni rasmi Waziri wa  Kazi Uwezeshaji Wanawake Wazee na Watoto Maudline Cyrus  Castico akimkabidhi Mtoto Salhia Muhsin zawadi maalum kwa kuingia kidato cha Tano Skuli ya Muzdalifa  katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto yatima yaliofanyika katika Viwanja vya Bakhresa Fumba Wilaya ya Magharibi B Unguja.  

PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.   

Na Salum Vuai, MAELEZO
MAKAMU wa Rais Samia Suluhu Hassan, amesema jamii ina wajibu wa kuwalea na kuwatunza watoto yatima badala ya kuwakwepa, kuwanyanyasa na kuwadhulumu.
Katika hutuba iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto Maudline Castico kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto yatima duniani huko Fumba, Samia amesema kuwapuuza yatima ni kubeba dhima kwa Mwenyezi Mungu.
Alifahamisha kuwa, ni lazima ndugu na wanafamilia wa wazazi wanaotangulia mbele ya haki, wakubali  kuwa walezi wa watoto wanaoachiwa kwa kila hali na kuwapatia mahitaji ya msingi ikiwemo elimu na kuwafundisha maadili mazuri.
Makamu wa Rais, alieleza kuwa, haijuzu kwa mtu mzima kupuuza umuhimu wa kuwalea na kuwatunza watoto yatima, ikizingatiwa kwamba kila mmoja atakutana na kifo wakati wowote, hivyo naye pia kuacha watoto nyuma yake.
“Unapomnyanyasa yatima wa Mungu, ukamnyima matunzo, na mara nyengine ukamdhulumu mirathi na haki zake wakati nawe pia una watoto, na ni mgeni katika dunia hii, je, ukifariki utaridhika watoto wako wanyanyaswe?”, alihoji Makamu wa Rais. 
Alisisitiza kuwa, jukumu la kuwalea na kuwatunza  watoto waliopoteza wazazi wao ni la kila mtu na wanapaswa kuwapa upendo, matunzo pamoja na elimu ambayo ndio mkombozi wa maisha yao kwa sasa na hapo baadae.
Alitumia nafasi hiyo kuipongeza jumuiya ya Muzdalifah inayolea watoto yatima ambayo ndiyo iliyoandaa maadhimisho hayo, kwa juhudi kubwa inazochukua kuwalea na kuwasomesha watoto.
Alisema hakuna kitu chenye thamani cha kumrithisha mtoto kama elimu, ambayo hata maandiko ya vitabu vitakatifu yanahimiza watoto kupatiwa rasilimali hiyo kwa jitihada zote.
Aidha aliwahimiza watoto kutekeleza wajibu wao wa kuishika elimu, akisema ndio ufunguo wa mafanikio katika maisha yao, sambamba na kuwapongeza baadhi yao waliofanya vizuri katika mitihani ya taifa ya kidato cha nne mwaka 2017.
Katika hatua nyengine, Makamu wa Rais alipaza sauti kuwakemea wanaume wasio na huruma wala aibu, ambao wamekuwa wakiwadhalilisha watoto kwa namna tafauti ikiwemo kuwabaka na kuwalawiti.
Kutokana na changamoto ya usafiri inayoikabili skuli ya Farouk wanayosoma watoto hao yatima, Makamu wa Rais aliwaomba wananchi wema wanaomiliki vyombo vya usafiri wa umma kuwasaidia watoto ili wawahi masomo.
“Watoto hawa tunaowadhalilisha ndio madaktari, walimu na viongozi wengine tunaowategemea watusaidie hapo baadae tutapoishiwa nguvu, hivyo ni vyema na busara zaidi kuwatendea mema sasa hivi ili nao watulipe wema tutakapokuwa hatujiwezi,” alisisitiza.
Hata hivyo, aliviomba vyombo vya usalama barabarani kuhakikisha kuwa wanaposimamisha daladala zinazojaza abiria kupindukia, pia wasimamishe gari zinazojaza wanafunzi kupita kiasi kwa kuzingatia usalama na afya ya watoto, na kuwachukulia hatua wenye gari hizo.
Katika risala yao, watoto hao walivitaka vyombo vya dola kuongoza juhudi katika kuwashughulikia watu wanaowadhalilisha na kuwapa adhabu kali ili kukomesha vitendo hivyo vinavyowanyima raha na kuwasononesha.
Aidha waliitaka serikali isaidie kuzipatia ufumbuzi changamoto zinazowakabili wahisani katika kuwalea hasa ikizingatiwa taasisi ya Muzdalifah haifanyi kazi kibiashara bali ipo kutoa huduma.
Naye Mwenyekiti wa Muzdalifah Dk. Abdalla Hadhar Abdalla, alisema taasisi yake itaendelea kufanya kazi kwa karibu na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwani kuwatunza watoto yatima ni katika mambo muhimu yaliyoasisiwa na kusimamiwa vyema na Rais wa kwanza wa Zanzibar marehemu mzee Abeid Amani Karume.
Aidha alisema mbali na kuwalea watoto yatima, pia wamekuwa mstari wa mbele kusaidia uimarishaji huduma mbalimbali za jamii, ikiwemo uchimbaji visima vya maji safi na salama, afya, ujenzi wa skuli na mambo mengine.
Hata hivyo, alitaja baadhi ya changamoto zinazowakabili ikiwemo uhaba wa dawa katika hospitali yao ya Kisauni inayohudumia jamii, akiiomba Wizara ya Afya kuangalia uwezekano wa kutatua tatizo hilo.
Maadhimisho hayo yalihudhuriwa pia na Mkuu wa Wilaya ya Kati Mashavu Sukwa Said, Mwakilishi wa Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Oguz Hamza Yilmaz, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, viongozi wengine mbalimbali na wananchi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.